Meli moja ya Uholanzi
iliyokuwa ikielekea katika
pwani ya Morocco kutoa
huduma ya utoaji mimba
kwa wanawake imezuiliwa
kuingia bandarini kwa
mujibu wa wanaharakati
walioituma nchini humo.
Kundi la wanaharakati hao
wanawake linasema kuwa
bandari ya Smir imefungwa
kabisa na meli za kivita
zinalinda doria eneo la
bandari hiyo.
Hapo jana Morocco ilisema
kuwa meli hiyo haijapewa
mualiko na mamlaka
zinazotambuliwa nchini
humo na hivyo ilikuwa
ikifanya shughuli hiyo
kinyume cha sheria.
Sheria za Morocco
zinakataza utoaji mimba
isipokuwa tu iwapo
maisha ya mwanamke
mjamzito yako hatarini.
Ibtissame Lachgar, ambaye
ni mmoja wa wanaharakati
wanaotetea haki ya utoaji
mimba amesema
wanawake wengi
wanalazimika kufanya
utoaji mimba kwa njia
zisizo rasmi ambazo ni
hatari.
0 comments:
Post a Comment