31 August 2012Nina amini kukaa kimya ni jibu tosha kwa mtu anaejifanya mjanja kumbe mjinga .pia huwa sibishani na ule msemo ukitukanana na mkichaa hakutokuwa na tofauti kati ya nyinyi wawili.
WEMA wewe kwangu mie ni bonge la superstar,hivyo wewe kuanza kujibishana katika magazeti na Snura ni sawasawa na kujishusha hadhi yako ya ustar ambayo mimi ninaamini unayo.
Kaa kimya Wema uone kama kuna sehemu ya mwili wako itabomoka,na wala usipoteze muda wako kuanza kusema vitu ambavyo umemsaidia kwani hata dini imekataza kumsaidia mtu halafu kumtangaza.
Nafikiri kwa hili wema utakuwa umejifunza kuwa hapa duniani hakuna kama mama,ninakumbuka mama yako alizungumza katika vyombo vya habari kuwa hauna rafiki wa kweli wewe,na ukamuwekea ukaidi ukamuona Snura ni rafiki mzuri kumbe hana lolote,alijifanya kujiliza pale mnafiki mkubwa.
Ndio ninamuita Snura mnafiki sababu kujiliza kote ila anasahau mazuri uliyomtendea na yupo kimbelembele kusema anazijua siri zako nyingi,huu ni unafiki kwangu mie.
Nijuavyo mie hata kama marafiki wakigombana lakini hawatoleani siri sasa iweje yeye aseme atazitoa siri zako hadi ushindwe kutembea mitaani,kuna kipya gani ambacho wewe Wema umefanya hapa duniani hakijawahi kufanyika?
Kikubwa ninakushauri angalia marafiki wema na sio kila msichana wa mjini wewe umuone rafiki yako na kumpa siri zako.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!