6 November 2014

 
 

IRINGA, Mwanamke mmoja mjini Iringa amtupa mtoto wake chooni mara baada ya kumzaa nyumbani.

Mama mmoja mjni Iringa anayetambuliwa kwa jina la Magdalena Limano mwenye umri wa miaka32, amemtupa mtoto wake chooni mara baada ya kumzaa.

 

Mshukiwa

Mtoto huyo wa kiume alizaliwa tarehe 4/11/2014 majira ya jioni na mama huyo na kuamua kumdumbukiza chooni, sababu alizotoa ni kwamba, kuna uwezekano mkubwa kuwa mtoto huyo si wa mume wake wa ndoa.

Mume wa mwanamke huyo yupo safarini kikazi na hana taarifa zozote za ujauzito wala taarifa za mke wake kujifungua na kitoto kuupwa chooni.


Chanzo cha habari kinasema kuwa, Magdalena uwa na tabia ya kumdanganya mumewe na kutoka na mabwana wengine pindi mumewe akiwa safarini kikazi.

Mtoto huyo aliyetupwa choon majira ya jioni mara baada ya kuzaliwa na kukutwa asubuhi ya tarehe 5/11 asubuhi akiwa analia ndani ya choo na majirani na kutoa taarifa.

Kwa juhudi za wasamalia wema, waliweza kumuokoa kichanga icho na kwa sasa mtoto ni mzima wa afya tele na yupo katika uangalizi mzuri wa hospitali huku mama yake mzazi akishikiliwa na jeshi la polisi akisubiri kufikishwamahakamani, kujibu shitaka la kujaribu kuuwa mtoto wake wa kumzaa mwenyewe.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!