Edson Cholbi do Nascimento Pele mtoto wa aliyekuwa mchezaji gwiji wa kusakata soka duniani Pele na kipa wa zamani amahukumiwa kifungo cha miaka 33 jela
Edinho mwenye umri wa miaka 43 aliyekuwa chezaji mpira wa miguu mstaafu
kwenye timu ya Santos amahukumiwa kwenda jela miaka 33 kwa makosa ya ufisadi na
fedha chafu zinazotokana na madawa ya kulevya.
Edinho kwa mara ya kwanza alikamatwa mwaka 2005 na alitumikia adhabu ya
kifungo kwa makosa ya kusafirisha madawa ya kulevya, pamoja na kuwa na mahusiano
na wauza madawa ya kulevya mjini Santos.
Mtoto huyo wa mfalme wa soka, Pele alikuwa akichezea club ya Santos nafasi
ya golikipa mwishoni mwa miaka ya 90.
Edinho, ambaye kwa sasa anafanya kazi ya ukocha akifundisha magolikipa
wa timu ya Santos, habari zinasema kuwa yeye ni mtumiaji mkubwa wa madawa ya
kulevya lakini amekana madai ya kuhusika na uhuzaji na kufanya biashara ya
kuuza madawa.
Vyombo vya habari vya Brazil havijaweza kumuhoji Edinho, ambaye jina
lake halisi ni Edson Cholbi do Nascimento.
Anatarajiwa ya kukata rufaa.
Edinho ni mtoto wa tatu wa Pele kwenye ndoa yake ya kwanza Pele
alipohamia New York kuchezea Cosmos Edinho alikuwa na miaka tano tu.
Mwaka 1995 Edinho ndiye aliyekuwa golikipa wakati timu ya Santos ilipocheza
fainali ya ligi ya Brazil, dhidi ya Botafogo .
Pele aliwahi kwenda kumtembelea motto wake, alipokuwa jela
mwaka 2006, na alisema: "Mungu akipenda, haki itapatikana, Hakuna hata
chembe ya ushahidi dhidi ya mwanangu"
0 comments:
Post a Comment