Sediuk aliondolewa na polisi katika tamasha la filamu la Canes wiki jana baada ya kuingia bila idhini
Mwanamume mmoja amekamatwa baada ya kumshambulia kwa makonde muigizaji maarufu duniani Brad Pitt usoni mwake katika sherehe ya ufunguzi wa filamu ya Maleficent mjini Los Angeles.
Mwandishi habari wa Ukraine Vitalii Sediuk - anayejulikana kwa kuwahahadaa watu mashuhuri duniani ,aliripotiwa kuonekana akivuka kizuizi na kumkumbatia Brad kabla ya kumpiga usoni.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa jina Vitalii Sediuk, alikamatwa na walinzi wa Brad baada ya kupambana naye na kukabidhiwa kwa polisi waliokuwa wanshika doria.
Vitalii Sediuk aliondolewa katika sehemu hiyo na polisi waliomfunga pingu
Pitt na mkewe Angelina Joli ndio waigizaji nyota katika filamu hiyo mpya ya Maleficent ambayo ilikuwa inazinduliwa na kampuni ya Disney.
Msemaji wa kampuni ya Disney iliyotengeza filamu hiyo alisema kuwa walisikitishwa na kitendo hicho na kwamba polisi wanafanya uchunguzi.
Sediuk alizuiliwa na polisi Jumatano usiku akisubiri kuachiliwa kwa dhamana ya dola 20,000.
Polisi walisema kitendo cha kijana huyo kilikuwa cha maksudi ingawa uchunguzi bado utafanywa.
Inaaminika kuwa Pitt alipigwa usoni ingawa polisi wanachunguza kisa hicho
0 comments:
Post a Comment