Raiya mmoja kutoka nchini China, ameshindwa kusafiri kurudi nchini kwake China yeye na familia yake, baada ya mtoto wake menye umri wa miaka mnne, kuonyesha ufundi wake wa kuchora picha mbalimbali za wanyama na watu kwenye passport ya baba yake.
Raiya huyo kutoka China amekwama Korea ya Kusini baada ya askari wa uhamihaji kushindwa kuthibitisha umiliki wa passport hiyo.
Raiya huyo aliyejulikana kwa jina moja tu la Chen, hatoweza kusafiri yeye na familia yake kurudi nchini kwake mpaka pale tatizo lake litakapo tatuliwa.
Picha hizi kwa mara ya kwanza zilitumwa na yeye mwenyewe kwenye mtandao ujulikanao kwa jina la Weibo, akiomba msaada wa jinsi gani ya kufanya ili aweze kurudi nchini kwake.
Picha zilizochorwa kwa peni nyeusi ni pamoja na paka, maua na watu wachache, na msanii huyo mwenye umri wa miaka minne hakuishia kuchora mauwa tu, bali aliongeza vitu vingine kwe ye picha ya baba yake kama vile ndevu na kuongeza nywele kidogo kama picha inavyo onekana.
0 comments:
Post a Comment