15 June 2014


 Bondia Mkongwe Iraq Hudu Amezikwa Leo jijini Dar es salaam

Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wakiwemo wanamichezo, leo wamejitokeza katika mazishi ya bondia wa zamani wa masumbwi ya kulipwa, Iraq Hudu (49).


Marehemu Hudu, maarufu kama "Kimbunga", alimefariki dunia Ijumaa mjini Dar es Salaam, amezikwa leo majira ya saa 10:00 alasiri katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Bondia huyo aliyewahi kutamba vilivyo katika ulingo wa masumbwi, alifariki alfajiri ya Ijumaa katika hospitali ya Hindu Mandal, akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi.


Hudu alizaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadae kwenda Dar es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari.

Baada ya hapo, alijiingiza katika masumbwi katika miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000, alipoacha.

Marehemu ameacha watoto watatu.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!