13 June 2014

Askari wa Jeshi la Taifa Somalia akiwa kwenye mafunzo nchini Somalia Machi 2012. Hivi karibuni Tanzania imekubali kutoa mafunzo kwa askari 1,000 wa Kisomali nchini Tanzania ili kuongeza uwezo wake wa kujihami.

Tanzania imekubali kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia kama sehemu ya jitihada zake za kuleta amani na usalama katika nchi ya Somalia, lakini baadhi ya viongozi wa Tanzania wameonyesha wasiwasi wao kuhusiana na kujiusisha kwa serikali ya Tanzania katika masuala ya Somalia. Wasiwasi wao unatokana na uwezekano wa kukaribisha mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa al-Shabaab.

Makubaliano hayo yanatokana na ombi la Rais aliyepita wa Somalia Sheikh Sharif Ahmed. Ombi ilo lilitolewa mwaka 2012. Baadae mwaka huu 2014 lilitolewa tena na Rais mpya ndugu Hassan Sheikh

Askari wapatao elfu (1000) wameombewa nafasi ya mafunzo na tayari kambi ya mafunzo imekisha andaliwa.

Mkurugenzi wa mawasiliano nchini Tanzania ndugu Salva Rweyemamu, amenukuliwa akisema “Tumesha andaa kambi ya mafunzo, ninapozungumza hapa ni kwamba kila kitu kipo tayari, tunasubiri wachague wanajeshi 1000 ili waje tuwape mafuzo”

"Tunataka kuwapa mafunzo ya kitaalam ili wawe na askari wazuri katika kudumisha usalama wa nchi yao na kuwapa fursa wananchi kushiriki katika masuala ya maendeleo ya nchi yao."

Waziri wa Ulinzi na Usalama wa Taifa ndugu Hussein Mwinyi alisema kuwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limekuwa likiongoza mafunzo na oparesheni za kulinda amani katika Afrika Mashariki na kwingineko katika jitihada za kujenga nguvu ushirikiano wa kikanda.

"Kwa kujenga nguvu na ushirikiano, JWTZ imetoa mafunzo ya kijeshi kwa maafisa wa kijeshi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Kusini," alisema maneno hayo katika hotuba ya bunge Mei 21.

Waziri alisema kuwa mwaka uliopita, JWTZ ilitoa fursa za mafunzo kwa askari na maofisa wa kijeshi kutoka Botswana, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Namibia, Shelisheli, Swaziland na Zimbabwe.

Pia alisema Tanzania ilishawai kutoa mafunzo ya awali kwa jeshi la Somalia ilifanya hivyo kutokana na ombi kutoka kwa Umoja wa Afrika, lakini hakusema mafunzo hayo yalikuwa ya namna gani na wala hakutaja idadi ya askari waliopewa hayo mafunzo hayo.

Alitaja operesheni nyingine ambapo Tanzania imechukua nafasi ya uongozi katika ujumbe wa kulinda amani, ikiwa ni pamoja Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lebanon na Sudan ya Kusini.

'Usalama wa Tanzania Kuwa Matatani?

Wakati serikali imesema ipo tayari kutoa mafunzo kwa askari wa Kisomali nchini Tanzania, wabunge na wananchi wameonyesha wasiwasi wao endapo serikali itakapo amua kutuma wanajeshi nchini Somalia, kunaweza kupelekea mashambulizi ya Al-Shabab kuenea mpaka nchini Tanzania.

Job Ndugai, naibu spika wa Bunge la Taifa la Tanzania, alisema ni hatari sana kwa usalama wa taifa kwa kupeleka majeshi nchini Somalia...

"Katika jambo hili nitakuwa mtu wa mwisho kukubali," aliiambia gazeti la Sabahi. "Angalia kile kinachotokea nchini Kenya. Serikali inapaswa kuwa makini na kulitafakari vema wazo la kupeleka majeshi nchini Somalia. Kama ikiwezekana ni bora kwa serikali ya Tanzania kuitisha vikao na mikutano kwa makundi yanayopinga uko Somalia."

Alisema askari wa Tanzania hawawezi kutumwa kwenda nchi yoyote bila idhini ya bunge kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama, na akasisitiza kuwa jambo au mpango kkama huo hauwezi kupitishwa na wabunge.

"Tanzania haipaswi kushiriki katika mpango huu kabisa. Nitakuwa mtu wa mwisho kukubali kupitisha muswaada wa kupeleka askari kutoka Tanzania kwenda Somalia"

Mbunge chama cha upinzani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ndugu Vincent Nyerere, aliiambia Sabahi kuwa “Tanzania inapaswa kufanya utafiti wake ili kujuwa kama kuna faida au thamani yoyote kwa Tanzania kushiriki katika mgogoro wa Somalia.” “Ni bora kujifunza kutoka kwa ndugu zetu wa Kenya,"

 "Hapo awali Kenya hawakuwa na uadui na Somalia, lakini kuingilia kwao kijeshi nchini Somalia kumepelekea mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara. Huu ni mtego na tunapaswa kujiondoa kwenye huu mtego."

Deus Kibamba, mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya Habari Tanzania (TCIB), alisema serikali inapaswa kuepuka kushiriki moja kwa moja katika mgogoro wa Somalia.

Alisema JWTZ iliundwa kulinda mipaka ya Tanzania na wananchi wake, lakini hali ya sasa ya kupeleka wanajeshi nchini Somalia kuna leta wasiwasi wa kuondoka kwa amani nchini. 

"Tunasikia tu kuhusu Makundi ya kigaidi kama Boko Haram uko Nigeria yanafadhiliwa na nchi au watu binafsi dhidi ya serikali iliyoko madaraka," aliiambia.

"Wakati tunaendelea kusaidia kile tunachokiita kulinda amani, polepole tunajenga uadui."

"Tanzania hivi sasa haipaswi kutumia zaidi rasilimali zake katika kushiriki kwenye kila vita au ugomvi unaotokea," alisema. "Tutajijengea maadui na itakuwa shida kubwa kwa nchi yetu."

Majeshi ya Tanzania Hayata Pelekwa Somalia

Rweyemamu amewahakikishia Watanzania kuwa serikali haita tuma askari kwenda Somalia na "Hakuna na haijawahi kupokea ombi lolote kutoka Somalia au Umoja wa Afrika".

Rweyemamu pia amewatoa wasiwasi kwamba Tanzania inaweza kuwavutia al-Shabaab kushambulia Tanzania kwa ajili ya kusaidia serikali ya Somalia.

"Kumbuka kuna serikali halali nchini Somalia," aliiambia Sabahi katika mahojiano Juni 5. "Tanzania haitakuwa eneo la vita nia yetu, ambayo ni nia ya kila mtu mwenye akili, ni kuona amani ikitawala nchini Somalia Ikiwa ni pamoja na al-Shabaab"

Source: sabahionline
Reactions:

0 comments:

Post a comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!