13 April 2014

Kwa wakazi wengi wa Dar es salaam soko la Kariakoo ndio sehemu muhimu kwa kujipatia mahitaji mbalimbali ya kila siku. Kuanzia nafaka, matunda na kila bidhaa inayohitajika kwa matumizi ya chakula kwa binadamu na baadhi ya mifugo.

Lakini kwa hivi karibuni kumefanyika mabadiriko makubwa kiasi mtu anaweza kupotea au kupatwa na mashangao wa muda, baada ya serikali ya jiji la Dare es Salaam wakishirikiana na uongozi wa soko ilo kuamua kuwaondoa wafanya biashara ndogondogo waliokuwa wamelizunguka soko na kufanya biashara zao na kujipatia riziki za kila siku.

Timu ya T-Mark iliamua kulifuatilia swala zima la kuondolewa kwa wafanyabiashara hao. Na kufanikiwa kupata sababu za kuondolewa kwa wafanyabiashara hao wadogowadogo.

Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara zao nje ya soko, wamekili kweli wameondolewa na wamehamishiwa ndani ya soko, lililoko chini ardhini.

Wafanyabiashara wengi wamelalamika kuwa uko walipo hamishiwa kuna upungufu mkubwa wa hewa na msongamano wa wafanyabiashara ni mkubwa kiasi cha kushinndwa kufanyabiashara vile walivyozoea. na wanachelea kuwa kunaweza kuzuka magonjwa ya kuambukizwa kutokana na msongamano na ukosefu wa hewa safi. Juhudi za mwandishi kukutana na uongozi wa soko la kariakoo zilishindikana kutokana na kutokuwa na namba za simu za wahusika.












0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!