13 April 2014

Mvua kubwa za siku mbili za sababisha zaidi vifo vya zaidi ya watu 14 na wengine wengi kupoteza makazi yao jijini Dar es Salaam.

Swala na Dua zikiendelea kuombwa kwa wakazi wa Dar es Salaam nchini Tanzania idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua kubwa inayoendelea nchini humo inahofiwa kupanda tayari na huku watu elfu nne na zaidi wameachwa bila makazi, baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Kulingana na shirika la hali ya hewa nchini humo mvua hiyo kubwa inatabiriwa kuendelea kunyesha kwa siku tatu zijazo. Hata hivyo tayari serikali ya Tanzania imefanikiwa kuwaokoa baadhi ya walikokwama na kuwahifashi katika maeneo yalio salama.

Amina abubakary amezungumza na Said Meck Sadiq mkuu wa mkoa wa dar es salaam na mwanzo anaelezea hali ilivyo.






























0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!