18 April 2014

Muigizaji wa filamu za kitanzania  (Bongo movie), Kajala Masanja hivi karibuni alipata shavu la nguvu baada ya kuibuka kuwa balozi wa wanawake Tanzania nzima kupitia taasisi ya Women Connect iliyopo jijini Dar.

Staa maarufu wa filamu hapa Bongo, Kajala Masanja.

Akizungumza na Ijumaa, mkurugenzi wa taasisi hiyo, Hafsa Semdaiya alisema wameamua kumchagua Kajala kwa kuamini ni kioo cha jamii na ni staa wa kwanza kuonesha moyo wa kuitikia wito kwani alianza kwa kutoa misaada kwenye kituo cha watu walioathirika na madawa ya kulevya.

“Kwa kweli kigezo kikubwa tulichokiona kwa Kajala ni moyo wake wa kujitoa na pia tumemuona ni kioo cha jamii na kama mwanamke anayejali, amekuwa mstari wa mbele kwenye kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye uhitaji,” alisema Semdaiya.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, taasisi hiyo inajihusisha na vitu vingi ila Kajala atahusika zaidi na kuchangisha fedha ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wenye vimbe mbalimbali.

Stori:global publisher

Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!