23 January 2014

Siku ukibahatika kutembelea Amerika na haswa jiji maarufu kwa wachezaji/waigizaji filamu, basi ni hakika utavutiwa kutembelea mtaa wa Hollywood Boulevard, mtaa ambao ni maarufu kwa alama za nyota zilizowekwa chini kwenye njia wapitao watu (walk of fame).


Lakini ni Ajabu mojawapo ukikaribia Kodak Theater utakuta moja la jina ambalo halikuwekwa ardhini kama majina mengine maarufu, unaweza kujiuliza jina ilo ni lipi? Usihangaike kulitafuta, jina lililowekwa ukutani badala ya ardhini kama majina mengi ni jina la mchezaji ngumi maarufu, Muhammad Ali.

Muhammad Ali, alipoitwa kwenye sherehe za kumtunukia umaarufu na jina lake liwekwe pamoja na watu wengine maarufu, aliwaomba waandaaji kwa kuwaambia kuwa kwenye jina lake kuna jina Muhammad (saw), jina ambalo ni la Mtume Mtukufu na si vema kuliweka ardhini likakanyagwa na watu.

Kwa heshima ya jina ilo la Muhammad, waandaaji wakakubali ombi lake na badala ya kuweka jina ardhini likawekwa ukutani. Na ndio jina pekee ambalo limewekwa kwenye ukuta. 6801 Hollywood Blvd.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!