24 January 2014


Mtoto Mwaru Lunard Sabil (9) aliyepigwa na kuumizwa vibaya na baba yake mzazi na kisha kulazwa katika Hospitali ya Wete, Pemba akipatiwa matibabu amefariki dunia na baba huyo bado anashikiliwa na Jeshi la polisi kutokana na tukio hilo.

Baba huyo mkazi wa Junguni Gando, Pemba, anadaiwa kumpiga na kumjeruhi vibaya hadi kumsababishia Mauti mtoto huyo kwa madai kuwa hafanani naye sura., hivyo si mtoto wake. Taarifa Zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Daktari wa Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Wete, Sada Juma Mbwana zilisema kuwa mtoto huyo amefariki dunia kutokana na maumivu makali aliyoyapata.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Shakhan Mohammed Shakhan, amesema Jeshi la Polisi linamshikilia baba mzazi wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 39 kutokana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu ijayo kujibu tuhuma zinazomkabili .

Pichani ni Mtoto Devotha Francis ambaye nae alifariki Dunia Mwaka jana baada ya Kucharangwa na Mapanga na Baba yake Mzazi huko Mjini Shinyanga
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!