Mwezeshaji wa mafunzo ya uboreshaji wa uandishi katika mitandao ya kijamii (blogu) kutoka mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) Simon Mkina katikati akimsikiliza kwa makini mwezeshaji mwezake Beda Msimbe wakati akitoa mfano wa uandishi bora wa habari za mitandaoni.
Na Francis Godwin Blogu-Dodoma MFUKO wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) umewataka wanahabari nchini kujikita zaidi katika uandishi wa habari za uchunguzi ili kuisaidia jamii na Taifa badala ya kuendelea kuandika habari zisizo na uchunguzi. Rai hiyo imetolewa leo na mwezeshaji wa warsha ya siku nne ya uboreshaji wa uandishi katika mitandao ya kijamii zikiwemo Blogu Bw. Simon Mkina wakati wa mafunzo hayo mjini Dodoma. Bw Mkina alisema kuwa pamoja na TMF kuamua kuanza kutoa ruzuku ya habari kwa blogu ila bado sehemu kubwa ya wanahabari nchini wamekuwa wakiripoti matukio zaidi badala ya kufanya uchunguzi na kuandika habari za kichunguzi ambazo ndizo zenye msaada mkubwa katika Taifa. Kwani alisema kuwa uandishi ambao utaleta mabadiliko katika vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii ni pamoja na kuwa na ukweli wa kutosha wa habari zinazoandikwa badala ya kutumia vyombo hivyo kuandika habari zisizo na maadili pamoja na habari zinazohatarisha usalama wa taifa . Hata hivyo alisema kuwa hivi sasa mitandao ya kijamii imekuwa ikitumia vibaya japo wanahabari wamiliki wa mitandao hiyo watajipanga na kujiunga na uandishi wa habari za kiuchunguzi na zinazozingatia maadili upo uwezekano mkubwa wa TFM kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa ruzuku kwa mitandao hiyo ya kijamii. Pia alisema kuwa wanahabari hao 20 ambao wamepatiwa mafunzo ya uandishi bora wa blogu ni chachu kwao kutumia mafunzio hayo kuleta mabadiliko ya kweli kwa mitandao hiyo ya kijamii ili iwe mfano mzuri kwa vyombo hivyo vya habari za mtandaoni. Katika hatua nyingi Mkina alitaka wanahabari hao na wengine ambao hawajapatiwa mafunzo ya uboreshaji wa habari za mkitandaoni ni vema sasa kurejea katika maadili . Huku mkufunzi wa mafunzo hayo Beda Msimbe alisema kuwa lengo la kuanzisha mafunzo hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika ni kutoka kuongeza ubora wa uandishi unaozingatia maadili katika mitandao hiyo . Alisema kuwa Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) umeanza kutoa mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza na kuwa washiriki wa mafunzo hayo ndio ambao watapatiwa ruzuku ya kwanza ya kufanya kazi ya uandishi kulingana na mawazo ya habari watakayowasilisha . Pia aliwaonya wanahabari hao kuacha kutumiwa na wanasiasa na badala yake kukubali kutumiwa na wananchi zaidi ili kuwasaidia katika kufikisha matatizo yao kwa viongozi wao. Msimbe alisema kuwa usalama wa wanahabari utaendelea kuwa hatarini iwapo wanahabari hawataheshimu maadili na kuendelea kutumika kwa kuchafua ama kufanya uandishi usio zingatia maadili. Kwa upande wake afisa miradi wa TMF Japheth Sanga aliwataka wanahabari hao mbali ya kuandika habari za uchunguzi kuhakikisha wanaheshimu sheria za nchi . Kwa upande wake Pia alisema TMF imekuwa ikisaidia vyombo vya habari na wanahabari nchini hivyo ili wanahabari hao kuendelea kunufaika na vema kujiunga kama kundi na kuomba fedha zaidi TMF. Alisema iwapo watafanya vema katika awamu hii ya kwanza wao kama TMF wataendelea kuwasaidia na ikiwezekano kutoa vifaa vya kufanyia kazi wanahabari hao. |
0 comments:
Post a Comment