26 August 2013

Msanii wa Kenya mwenye wimbo wa “Sina Beef” aitwae Maleek amefanya kitendo cha kusikitisha sana baada ya kutangaza motto wake amefariki na kuomba michango hali halisi ikiwa motto wake mzima kabisa.
Ilivyoanza msanii huyo ali-post katika ukurasa wake wa facebook kua Binti yake mgonjwa sana, na baada ya siku mbili aka-post tena kua binti yake amefariki tena kwa quote na mistari ya Biblia kila baada ya muda mfupi akionyesha ni jinsi gani ameguswa na msiba huo (Feki).

                    MALEEK

Wa-kenya wenzie wakawa wamemchangia pesa na walipokwenda nyumbani kwake ili kushiriki nae msiba walishangazwa kumkuta marehemu akicheza kama kawaida na katika njema kabisa.
Watu wakapandwa hasira sana baada ya kugundua mchezo mzima wampigia simu ambapo akawa hapatikani baada ya muda wakampata kwa simu na kuanza kuwaomba msamaha akidai kua ni SHETANI TU ALIMPITIA na akawaahidi kua atarudisha pesa zote ambazo ni zaidi ya LAKI 3 za Kenya.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!