26 November 2012

Snura Mushi. Mwigizaji na mwimbaji. Alikuwa shosti mkubwa wa mwigizaji mwenye matukio mengi Bongo, Wema Sepetu. Walizinguana miezi kadhaa iliyopita, ushosti ukafa. Kila mmoja alichukua hamsini zake, bifu zito likaanza kutokota kati yao. 
Kila mmoja alitaka kumuumbua mwenzake. Eeeh si mlikuwa mkifanya mengi pindi mlipokuwa marafiki? Si mlikuwa mkitunziana siri? Sasa ilikuwaje mkaanza kumwaga mchele kwenye kuku wengi? Hahahahaha… ustaa bwana! Mlioneshana ubabe wa maneno, bifu lenu likatawala magazetini. 
Hivi karibuni nimesikia upo katika mchakato wa kuwaomba radhi watu ambao unahisi umewakosea, ni wazo zuri. Hongera sana lakini ninachokiona umechelewa kidogo.
Nakumbuka pindi ushoga wako na Wema ulipovunjika, kuliibuka maneno mengi. Mengine yakisikika kutoka katika kinywa chako na mengine ukinukuliwa na watu pindi wakimuona mhusika uliyemzungumzia, mwisho bifu linaendelea kukua bila ya wewe kujua ndiyo chanzo.
Kumbe kama ungewaza haya toka zamani, pengine msingefikia hapa mlipo sasa hivi. Yawezekana mngekuwa mmeombana radhi na mmepatana, maisha yakaendelea kama kawaida.
Ilifika wakati ulishawishiwa na kikundi cha watu eti wakudhamini ili utengeneze filamu ambayo itakuja kupewa jina la ‘Uozo Wa Super Star na wewe ulikubali. Ulifanya mahojiano katika kituo kimoja cha runinga na kubainisha kama filamu hiyo inamlenga Wema waziwazi.

 Wema alisikitika sana, alisema umemdhalilisha. Hakuwa na jinsi zaidi ya kusema anamuachia Mungu. Kumbe pengine kibinadamu ulikuwa na nafasi ya kufunguka vile mkiwa wawili, yakaisha. Pale kwenye runinga mamilioni ya Watanzania ‘walijinoma’ bifu lenu.
Yote kwa yote, bado nakupongeza, Uamuzi wako wa kuomba radhi uliofikia ni mzuri. Inaonesha kuna kitu umejifunza kama si kushauriwa na watu. Nimesikia kuwa umeshamuomba radhi Chidy Classic ambaye naamini ndiye aliye kuunganisha na Wema.
Kimsingi kwa kuwa umetambua ulipojikwaa, nikupongeze kwani ni maamuzi mazuri. Waombe radhi wote hadi kina Lady Na na wengine wote ambao ni marafiki wa Wema. Watakuelewa tu. Huo ndiyo ubinadamu.
NA SHAKOOR JONGO

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!