12 April 2012

Naibu waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma.

Naibu Waziri wa Ujenzi Dkt. Harrison Mwakyembe amewatia kiwewe wabunge wanaohudhuria kikao cha Bunge wakati aliponyanyuka kwa ukakamavu mkubwa na kujibu maswali aliyoulizwa na wabunge.
Dkt. Mwanyembe aliwaamusha wabunge na kumpigia makofi mengi pale alipoamriwa na Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kuamka na kujibu maswali ya wabunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni mjini Dodoma.
Kabla ya kujibu maswali hayo Dkt. Mwakyembe alisema kuwa yeye kwa sasa amepona na anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpa tena uhai.
Vile vile Dkt. Mwakyembe alisema kuwa anawashukuru wabunge, wananchi wote wa Tanzania, Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Rais Jakaya Kikwete kwa kujali uhai wake.
Alisema kuwa Rais Kikwete alikuwa mtu wa kwanza kutaka yeye apelekwe India kwa matibabu baada ya kuona hali yake ilikisuasua na kuonyesha hali ya hatari sana.
Akijibu maswali Bungeni Dkt. Mwakyembe alisema kuwa masuala ya utaalamu katiak ujenzi wa barabara ulikuwa ni jambo la muhimu sana.
Dkt. Mwakyembe alisema kuwa baadhi ya wabunge wanaonekana kuchukizwa na misemo ya kitaalam kama vile upembuzi yakinifu na kadhalika, lakini maneno hayo yanaonywesha kuwa serikali inatekeleza mambo ya kimaendeleo kwa utaalam mkubwa ndipo misemo hiyo inapoibuka.

Kwa hisani ya www.dewjiblog.com /www.dodoma-yetu.blogspot.com 

Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!