12 May 2012


 •  PAMOJA KWAMBA HAUKO NAMI KIMWILI LAKINI KIROHO TUKO PAMOJA MAMA, NINAKUPENDA,NINAKUHESHIMU,NINAKUTHAMINI NA NITAKUJALI MILELE, MALEZI YAKO HEKMA ZAKO NA BUSARA ZAKO NDIO ZIMENIFANYA MIMI KUWEZA KUSIMAMA NA KUTIZAMA FAMILIA BILA YA UWEPO WAKO MAMA.
  HAKIKA WEWE NI MWANAMKE WA KIPEKEE KATIKA MAISHA YANGU, TULIKUWA ZAIDI YA MAMA MTOTO WAKE.ULIKUWA RAFIKI YANGU WA UKWELI AMBAPO HADI LEO HII SIJAPATA RAFIKI WA UKWELI KAMA WEWE.
  ULIKUWA UKINIAMINI KWA KILA NILILOKUWA NIKIKUELEZA MAMA,NA ULIJENGA IMANI NA MIE KWA KUWEZA KUNIELEZA YA MOYONI KWAKO MAMA YANGU.ULIKUWA UKIAMBIA UKWELI PALE NILIPOKOSEA BILA YA KUPITIA KWA MTU YOYOTE.
  NINAKUMBUKA PALE ULIPOKUWA UKINIAMBIA MWANAMKE JASIRI NI YULE MWENYE KUJITAFUTIA MWENYEWE BILA YA KUSUBIRI KULETEWA,SITAACHA KUKUSHUKURU KWA YALE MANENO YAKO ULIYOKUWA UKINIAMBIA SOMA MAMMY HAYA MAMBO MENGINE YOTE UTAKUTANA NAYO NA YATAKUCHOSHA TU.
  KWANINI NISIKUITE SUPER MAMA KATIKA HII DUNIA HASA PALE ULIPOAMUA KUSIMAMA WEWE KAMA WEWE KWA KUNILEA NA KUNISOMESHA,NA KUHAKIKISHA MALENGO YANGU YANATIMIA.
  MAMA SIKUKUANGUSHA MPENZI WANGU,NILIMALIZA CHUO SALAMA,NA KILE ULICHOKUWA UKINIASA CHA KUTOKUZAA BILA YA KUOLEWA NINAKUPIA NIMETIMIZA,SASA NINAE BINTI WA MIAKA MIWILI NA MIEZI MIWILI AMBAYE NIMEMPA JINA LAKO.NA NINAZIDI KUMUOMBA MUNGU NITIMIZE NA MENGINE ULIYOKUWA UKINIHUSIA YASINITOKEE KATIKA MAISHA YANGU,INSHALLAH MAMA HAKIKA MUNGU ATANISIMAMIA KWA KUNIONDOLEA KILA AINA YA MITIHANI .
  SIWEZI KUKOSOA KAZI YA MUNGU, ILA NAONA UMEONDOKA MAPEMA SANA,! INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU AKUONDOLEE ADHABU ZA KABRI,NA ALITIE NURU KABURI LAKO,AKUPE KAULI NJEMA NA MALAIKA  INSHAALLAH  NA AKUPE KAULI THABITI SIKU YA HUKMU MAMA YANGU.
  HAPPY MOTHERS DAY!!!
Reactions:
Categories:

1 comment:

 1. Pole sana Mpenzi may ur mum's soul R.I.P am sure she's so proud of you and she's watching over you.

  ReplyDelete

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!