2 January 2015

Watu 36 wamepoteza maisha na wengine kiasi ya 40 kujeruhiwa kotokana na mkanyagano katika hekaheka za kusherehekea mwaka mpya nchini China.

 Tukio hilo lilitokea wakati umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika katika uwanja wa Chen Yi Square. Shirika la habari la China Xihnua limemnukuu aliyeshuhudia mkasa huo akisema watu walikuwa wakitaka kujipatia kuponi ambazo zilionekana kama fedha aina ya dola ambazo zilikuwa zikirushwa kutoka katika dirisha kutoka gorofa ya tatu ya jengo moja.

Hatari Ilianza Kabla ya Kuwadia 2015

Serikali ya China iliosema umma huo wa watu ulianza kukanyagana mapema kabla ya kutimia usiku wa manane, katika mji huo wenye mchanganyiko wa watu. Tukio hilo linaelezwa kuwa baya zaidi kutokea tangu mwaka 2010, baada ya kuzuka moto katika jengo lenye makazi ya watu na kusababisha vifo vya watu 58.

Chanzo cha mkanyagano huo bado hakijafahamika lakini chombo cha habari cha serikali na baadhi ya walioshuhudia wanasema kwa sehemu fulani kadhia hiyo imesababishwa na watu wakiwania kujipatia fedha zilizoonekana kama ni sarafu halisi.

FedhaBaandia Zilirushwa Kama Theluji

Bwana mmoja kati ya watu 47 waliofikishwa hospitali kwa ajili ya matibabu alisema fedha bandia zilikuwa zinarushwa kutoka katika jengo moja ikiwa sehemu za sherehe za mkesha wa mwaka mpya. Watu walikuwa wakikimbia kwenda kuchukua kuponi. Alisema mtu huyo ambae alijitambulisha kwa jina la ukoo la Wu.

Bwana mwingine Cui Tingting, mwenye umri wa miaka 27 alisema alifanikiwa kupata kiasi fulani cha kuponi hizo lakini alizitupa baadae baada ya kugunduka kuwa zilikuwa fedha bandia. "Ulikuwa ukatili sana. Watu waliokuwa mbele yetu walikuwa tayari wamelala katika sakafu, na baadhi ya watu walikuwa wakiwakanyaga,"alisema majeruhi huyo.

Televisheni ya serikali ilinukuu wazungumzaji wengine wakisema fedha hizo bandia zilikuwa zikitiririka chini mithili ya theluji.

Kauli ya Polisi Kuhusu Mkasa

Jeshi la polisi mjini Shanghai lilisema halikuweza kuthibitisha kama fedha hizo bandia ndizo zilizosababisha mkanyagano, na kuongeza kwamba uchunguzi unaendelea huku likiwataka wananchi waendelee kuwa watulivu kwa wakati huu.

Milango ya vioo ya jengo ambalo limetajwa kutoa fedha hizo bandia imeonekana kufungwa Alhamis hii, ingawa ishara za mabaki yalionesha kulikuwa na shamrashamra kwa wakati uliopita zinaonekana katika sakafu yake.

Kwa kupitia televisheni ya taifa ya nchi hiyo Rais Xi Jinping ameitaka serikali ya Shanghai kutafuta chanzo cha tukio hilo haraka iwezekananvyo na kuamuru serikali katika maeneo yote nchini China kuhakikisha kwamba mkasa kama huo hautokei tena.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!