Watoto wa mtaani wakimuonyesha Mwandishi jinsi wanavyoishi na wanavyokula mkate kwa kuuloweka na maji, ili waweze kula.
Jina "Watoto wa Mitaani" ni jina maarufu sana, haswa kwa wakazi wa miji mikubwa nchini Tanzania. Lakini tunashindwa kujiuliza mara mbili, je Mitaa ina uwezo wa kuzaa watoto, kiasi wapatikane watoto wa mitaani?
Tatizo la watoto wanao zurura mitaani, limekuwa kubwa sana nchini Tanzania, kiasi wamepewa jina la Watoto wa Mitaani, kana kwamba mitaa ndio wazazi wa hao watoto.
Serikali na wananchi wanapaswa kuliangalia upya swala la watoto hawa, kwa sababu watakapoachwa bila kupewa misaada ya kijamii, kama vile kulelewa kwenye vituo vya kulelea watoto, kitakacho tokea baada ya miaka michache ni kuzalisha majambazi na vibaka na makahaba watakao sumbua jamii inao wazunguka.
Tunaiomba serikali kupetia taasisi zake na wizara husika, waliangale na kuchukuwa hatua ili kuwanusuru hawa watoto, ili Taifa lisije pata hasara kwa kupoteza nguvukazi na rasilimali yake.
0 comments:
Post a Comment