Shirika la kutetea haki za binaadamu limesema, wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanaolinda amani nchini Somalia wamewadhalilisha kingono wasichana na wanawake wa kisomali wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mogadishu.
Vikosi hivyo kwa wakati tofauti vimejihusisha na ubakaji wa wanawake na wasichana wadogo wa miaka 12 na kuuza chakula kwa ngono, shirika la Human Rights Watch lilisema katika ripoti siku ya Jumatatu.
"Baadhi ya wanawake waliobakwa walisema kwamba wanajeshi waliwapa chakula au fedha baadaye katika jaribio la wazi kuliita shambulio hilo kama biashara ya ngono," ripoti ya HRW ilisema.
Hakukuwa na ushughulikiaji wa haraka kutoka kwa AMISOM, ambayo wanajeshi 22,000 walitoka katika mataifa sita wamekuwa wakipigana kwa pamoja na vikosi vya serikali ya Somalia dhidi ya al-Shabaab tangu mwaka 2007.
Wanawake walio hatarini kwa kiasi kikubwa wanatoka katika makambi huko Mogadishu, wakikimbia Somalia vijijini wakati wa njaa kali mwaka 2011.
Wanajeshi wa AMISOM, "wakitegemea wanaoingilia kati wa Somalia, wametumia mbinu kadhaa, ikiwa ni pamoja na misaada ya kibinadamu, kuwalazimisha wanawake na wasichana katika mazingira magumu kufanya ngono," ripoti hiyo ilisema, ikizingatia ushahidi wa wanawake na wasichana 21.
"Pia walibaka au vinginevyo kushambulia kingono wanawake waliokuwa wakitafuta msaada wa matibabu au maji kwenye makambi ya AMISOM," ilisema ripoti ya kurasa 71, "'Nguvu Walizonazo watu hawa Kwetu': Unyonyaji wa Kingono na Unyanyasaji wa Vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia".
Mdogo kabisa kuhojiwa alikuwa na miaka 12, aliyesema alibakwa na askari wa Uganda.
Wanawake kadhaa walieleza jinsi walivyokwenda kwenye kambi ya AMISOM kutafuta dawa kwa ajili ya watoto wao wagonjwa.
"Matokeo yalileta wasiwasi mkubwa kuhusu unyanyasaji wa wanajeshi wa AMISOM dhidi ya wanawake na wasichana wa Somalia ambayo yanaonyesha tatizo kubwa sana," HRW aliongeza.
Ni katika matukio mawili tu ambapo wanawake walioongea na HRW walipeleka malalamiko yao polisi, kwa sababu "walihofia unyanyapaa, kisasi kutoka kwa familia, polisi, na kundi la uasi wa Kiislamu la al-Shabaab".
"Wanajeshi wa Umoja wa Afrika na uongozi wa kisiasa wanatakiwa kujitahidi zaidi kuzuia, kutambua, na kuadhibu unyanyasaji wa kingono unaofanywa na vikosi vyao," alisema Mkurugenzi wa HRW Afrika Daniel Bekele.
"Wakati tatizo lingine la chakula linaongezeka kwenye makambi ya wasio na makazi Mogadishu, kwa mara nyingine wanawake na wasichana wasio na uhakika wa chakula na dawa. Hawapaswi kuuza miili yao ili familia zao ziishi," Bekele alisema.
Wakati huo huo Umoja wa Afrika (AU) imeidhinisha timu ya uchunguzi kuchunguza tuhuma kwamba wanajeshi wa Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia waliwabaka wanawake na wasichana wadogo wa miaka 12 na kufanya biashara ya chakula kwa kufanya ngono nchini Somalia.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Nkosazana Dlamini-Zuma aliagiza uchunguzi Ijumaa (tarehe 17 Oktoba) katika kujibu ripoti ya Human Rights Watch (HRW) mwezi Septemba ambayo ilituhumu wanajeshi wa AMISOM kwa kuwabaka wanawake.
Timu hiyo ya uchunguzi inaundwa na wanaume wawili na wanawake wawili wanaotoka Ghana, Tanzania na Zimbabwe na wana ujuzi mzuri wa kutekeleza "jukumu muhimu sana", AMISOM ilisema katika taarifa.
Timu hiyo "itafanya uchunguzi katika tuhuma mahususi za unyonyaji na unyanyasaji wa kingono zilizotolewa dhidi ya watumishi wa AMISOM, hususan vikosi vya Uganda na Burundi", ilisema taarifa hiyo.
Timu hiyo "itashughulikia mahitaji ya wanaodaiwa kuwa waathirika na mashahidi muhimu pamoja na matakwa ya wote wanaohusika ili kupata ukweli kuhusu tuhuma hizo."
Awali AMISOM ilielezea tuhuma hizo kuwa matukio "yaliyojitenga" na kuiitaja ripoti ya HRW "yenye upungufu na isiyo ya haki".
Wanawake kadhaa waliotajwa kwenye ripoti ya HRW wanaeleza jinsi walivyokwenda katika kambi ya AMISOM kutafuta dawa kwa ajili ya watoto wao wagonjwa, lakini badala yake walilazimishwa kufanya ngono.
Wanawake wengi walio katika mazingira magumu walitoka katika makambi ya waliopoteza makazi nchini mwao huko Mogadishu, waliokimbia Somalia vijijini wakati wa njaa kali mwaka 2011.
Uchunguzi utakamilika ifikapo tarehe 30 Novemba pamoja na ripoti itakayoabidhiwa kwa Dlamini-Zuma.
"Matokeo na mapendekezo yatatangazwa kwa umma... kwa kuzingatia kwanza ulinzi wa mwathirika, haki za wakosaji wanaodaiwa pamoja na umuhimu wa shughuli wa AMISOM," ilisema taarifa ya AMISOM.
0 comments:
Post a Comment