Aliyekuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela, amefariki dunia Usiku wa tarehe 5 Dec 2013 akiwa na umri wa Miaka 95.
Mandela ambaye alitumikia jela miaka isiyopungua 27 alichaguliwa kuwa Rais wa Kwanza Mweusi katika nchi ya Afrika Kusini, na uchaguzi huo, ulihitimisha serikali ya Kibaguzi ya wakati huo kuwa sasa ni wakati wa kuishi pamoja na ni muda wa kusameheana.
Nelson Mandela,, hivi karibuni alikuwa akisumbuliwa na maradhi yaliyopelekea kulazwa mara kwa mara hospitali.
Nelson Mandela, Atakumbukwa kama Mwanasiasa ambaye ameweza kuwaunganisha wananchi wa Afrika kusini na kuwa kitu kimoja na kuwa mfano wa kuigwa kwa wanasiasa duniani.
- Jina: Nelson Rolihlahla Mandela
- Amezaliwa: July 18, 1918 (Umri 95), Mvezo, Afrika Kusini
- Wake zake: Graça Machel (m. 1998), Winnie Madikizela-Mandela (m. 1958–1996), Evelyn Mase (m. 1944–1958)
- Watoto zake: Madiba Thembekile Mandela, Makaziwe Mandela, Makgatho Lewanika Mandela, Makaziwe Mandela, Zenani Mandela, Zindziswa Mandela
- Amefariki: 5 December 2013
0 comments:
Post a Comment