Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe mwishoni mwa wiki iliyopita
(Jumamosi, 23 na Jumapili, 24 Machi 2013) alitembelea baadhi ya shughuli za miradi
mbalimbali zinayofanywa na Watanzania
waishio Leicester and Northampton kwa lengo la kufahamu mafanikio na changamoto
zao.
Akisindikizwa na Afisa
wa Ubalozi, Bw. Amos Msanjila, Balozi alipenda kufahamu nini mahitaji ya Watanzania hao ili kuweza
kujenga mkakati muafaka wa kuwatia moyo na kuwashirikisha wananchi hao kujenga
nchi.
Akiwa Leicester
alipata fursa ya kutembelea kituo cha redio ya jamii ya mji huo na kufanyiwa
mahojiano ya moja kwa moja kwa Kiswahili na Mtangazaji wa redio hiyo, Bw. Omar
Hussein. Redio hiyo inasikika moja kwa moja katika maeneo yote ya Leicestershire na vitongoji vyake.
Aidha Balozi Kallaghe
alitembelea kiwanda kidogo cha
usindikaji wa vyakula na viungo kinachomilikiwa na mfanyabiashara mwenye asili
ya Tanzania cha Jalpur Millers. Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho Bw. Deepen J. Pau
alimwambia Balozi kwamba Kampuni yao ina mipango ya kuwekeza zaidi Tanzania.
Baadae Mheshimiwa
alitembelea kituo cha kuratibu usafirishaji wa mizigo mbalimbali kwa makontena
kwenda nchi za Afrika Mashariki na hasa Tanzania. Pamoja na kuonyeshwa shughuli
mbalimbali zinazofanyika hapo, Balozi alipata pia fursa ya kuzungumza na wajasiliamali
Bw. Abdul Nasser Hamed wa Zanzibar
Driving School na Mussa Issa Mussa wa BMA Store and Shipping Agency.
Alipata pia fursa ya kutembelea mgahawa wa biriyani wa Maalim Hamis na kukutana na
mpishi huyo maarufu kabla ya kukutana na Watanzania wachache, hasa viongozi wa
Jumuiya ya Watanzania ya Leicester.
Siku ya Jumapili
Balozi alitembelea Jambo Hair Salon na baadae kukutana na viongozi wa
watanzania wachache kwenye Mgahawa wa Kass’s Grill unaomilikiwa na kijana wa
kitanzania Kasongo Mohamed. Pamoja na kupata chakula cha mchana kwenye mgahawa
huo, Mheshimiwa alifanya na mazungumzo na watanzania hao na kusisitiza umuhimu
wa mshikamano na moyo wa kuunga mkono biashara za watanzania wenzao.
Mheshimiwa ataendelea
kutembelea miji mbalimbali hapa Uingereza na kujionea shughuli zinazofanywa na
Watanzania kila atakapopata fursa ya kufanya hivyo.
0 comments:
Post a Comment