Tetesi zinaweza kuwa za ukweli au pengine zikawa ni story za kujitungia
Lakini tetesi zinasema kuwa Matonya alipigiwa simu na wazee wa fitna mara tu waliposkia kuwa atashiriki onyesho la miaka 13 ya JayDee, wakamwambia aachane na hiyo show na kuwa watampa hela ambayo angelipwa kwenye show hiyo.
Na pia wangemuandalia show yake mwenyewe kubwa zaidi ya hiyo miaka 13 ya JayDee
Hizo ni fununu, ambazo hazina uhakika.
Lakini tukirudi upande wa Matonya ambae alishapokea mpaka malipo ya awali na kukubali kufanya show baadae akachomoa ni kama ifuatavyo.
MATONYA: Kaka kumbe tarehe ni lini kumbe:
CAPTAIN: Ni Ijumaa tar 31 May 2013 kaka mwezi ujao. Tutakuwa na Linah, Jay, Barnaba, Matonya, TID, hamza Kalala
MATONYA: Kaka kumradh sana kuimba na band kwasasa sitoweza manake mtaitaji mandalizi makubwa ili nifanye kazi vzr_ningeomba nitizamwe ktk kazi ingine bro kumradh sana
CAPTAIN: Du! Nshatangaza ilikuwa kaka lakini sawa. Je ntapata ile hela kka nilipe wengine ndg yangu
MATONYA: Aisee hata nimekosa raha kukujuza iliswala br_kesho satano mtampa yule rafkiangu anaitwa pizon_walikuja kuleta ile pesa yagari kwaio wataileta apo apo oficen
CAPTAIN: Sawa kaka usijali, Nitashukuru akiileta ili huku nisipate lawama
MATONYA: ok bro
Mara kimyaaaaaaa....... baada ya siku mbili tatu maongezi yakaendelea
CAPTAIN: Naam kaka mzigo haujaletwa. Tafadhali ileteni tu hiyo hela ya watu kaka mi napewa lawama isitoshe we ni ndugu yangu usikubali hela ndogo iharibu.
MATONYA: Gadna aiwezi kuwa ivyo_kuna mapungufu kidgo nayaweka sawa uipate kumradh sana brother
CAPTAIN: Asante
Siku ikapita tena
MATONYA: Kaka kdg kunamisteki nimecheza,, lakini wiki hii haitapita mtakuona bro nimekwama kaka lakini ntajua cha haraka
CAPTAIN: Sijaelewa kaka ni laki **** tu kunirudishia nduguyo nilipe wasanii wengine kwani kuna tatizo au
MATONYA: Bro naskia haya - skutaka hata kuku2mia msg mlitaka ni2we namzigo 2 ila kunambio kdg zimekwamisha nikaona bora kukujuza kuliko kukaa kimya bro tatizo haliwezi
CAPTAIN: Sawa we ni ndugu yangu, basi nisaidie tu irudi hiyo advance niliyokupa ili uniepushe na lawama huku kaka. Au niende kwa bimkubwa Tanga nikalalamike? Ha haaaa haaa
CAPTAIN: Fanya hivyo mdogo wangu nilitaka uwepo ktk show kwa upendo tu lakini haijawa, basi nisaidie tu kurudisha hiyo advance maana nadaiwa na wasanii wengine niwape. Au sio?
MATONYA: Kaka nibendi ndio haya yangu kwasasa nastaki kuharibu kaziyako bora niwe mkweli.. Naswala lako halitoki kichwani bro
CAPTAIN: Sawa jamaa yangu, basi nisaidie ile advance irudi ili niweke mambo sawa huku, mimi sina mdhamini mpaka leo aliyetoa hela, najitegemea tu mfukoni, naomba nirudishie nilipe wengine..Au namoro matonya we ni ndugu yangu?
MATONYA: Sawa brother mtalisimamia soon nikuweke sawa sawa brother - akuna litakalo shindikana kaka amini 2
CAPTAIN: Utarudisha lini nipe uhakika kaka, niko na shida
Adavance ilitoka tangu mwishoni mwa mwezi April
Mazungumzo ndio kama hayo mmeyasoma
Mpaka blog inaingia mitamboni leo, advance haijarudishwa na hakuna jibu la kueleweka.
Wazee wa fitna kama zile tetesi ni kweli kuwa mmemzuia Matonya asifany hii show ya miaka 13 ya JayDee, na hela ameshaitumia! Kwanini msimsaidie kuirejesha mambo yaishe??
Story na picha toka katika blog ya jide
0 comments:
Post a Comment