6 January 2015

Mtangazaji Maarufu wa Kipindi cha Vichekezo kwenye Luninga ya BBC QI Stephen Fry Mwenye umri wa miaka 57, ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa ataolewa na mwanamume mwenzio, mchekeshaji Elliott Spencer mwenye umri wa miaka 27.

Stephen Fry amenukuliwa akisema kuwa ana furaha kubwa sana, baada ya kuweka appointment kwa msajili wa ndoa mjini Dereham, Norfolk, mji ulio karibu na mji aliokulia.

Stephen Fry Miaka 57 Akiwa na Mpenzi Wake 
Elliott Spencer Miaka 27, Anayetarajia Kumua Hivi Karibuni.

Stephen Fry, zaidi ya kuonyesha kuwa ni mwenye furaha, lakini anasumbuliwa sana na msongo wa mawazo na ugonjwa wa akili unaojulikana kitaalam kama Bipolar Disorder.

Msaidizi wake amesema kuwa swala la boss wa kuolewa na kijana mdogo wa kiume ni swala binafsi, kinachoangaliwa ni kuwa "Stephen Fry ni mwenye furaha na mwenye kujivunia uhamuzi wake huo.

Stephen Fry Akiwa na Mpenzi Wake Elliott Spence Kwenye Matembezi ya Jioni.
 
Tarehe ya ndoa yao bado haipo wazi kutokana na mambo mengi yanayomkabili mtangazaji huo.

Source: Mirror | BBC
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!