5 January 2015

Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 ambaye alishiriki mashindano ya Mwanamke mwenye Makalio mazuri zaidi nchini Brazil (Miss BumBum) amelazwa hospitali na kufanyiwa upasuwaji wa dharura, baada ya geli zilizotumika kwenye kumuongezea ukubwa wa makalio, kuozesha nyama za matako na mapaja yake.

Mwanamitindo huyo Andressa Urach, miaka 27, alikuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo maarufu nchini Brazil, yaliyofanyika mwaka 2012.

Brazili ni nchi ambayo wanawake wengi wanapenda kufanyiwa ukarabati wa maungo yao, ili waonekane warembo na wenye kuvutia, ikiwa nyuma kwa Marekani (USA).

Mwanamke huyo alikuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi kwa karibu mwezi mzima, na kulazimika kufanyiwa upasuwaji ili kuokoa maisha yake.

Picha hizi zinaonyesha ni kiasi gani hali yake ilivyokuwa mbaya kabla ya matibabu.

Mwenyewe anasimulia kuwa alidungwa sindano na kuingizwa aina mbili za gel maalumu kwa ajili ya kuongezea ukubwa wa makalio (hydrogel na PMMA).

Lakini kile alichokitarajia, kilikuwa tofauti, kwa sababu mwezi wa Julai, alianza kupatwa na maumivu. Alipofikishwa hospitali, waliondoa karibia nusu lita ya hydrogel kutoka kila moja ya mapaja yake.


 

Reactions:

0 comments:

Post a comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!