13 June 2014






Kombe la Dunia ndiyo limefika, tungependa kufafanua na kuweka sawa mambo kadhaa ili usiulize swali la kijinga.
1.    Hakutakuwepo na mazungumzo yasiyohusu soka wakati wa kipindi cha kawaida ama ziada cha mechi na hasa wakati wa penati.
2.    Utazishabikia timu nitakazokuwa nazishabikia tu! Utatabasamu pale tu timu ninayoishabikia itakapokuwa inashinda na utashangilia "goliiiiii" wakati goli kweli limetinga nyavuni.
3.    Wataarifu marafiki zako wasifunge ndoa, wasizae, wasiugue wala wasife katika kipindi cha Kombe la Dunia! Hatutahudhuria hayo!
4.    Hili ni Kombe la Dunia! Hakuna Asenali, ManU wala Barcelona. Huwa linachezwa mara moja kila baada ya miaka minne, kwa hiyo usiniulize kama ni mechi sawa na zilizochezwa wiki zilizopita.
5.    Tutatizama soap, reality show, romantic, African na sinema za Kiafrika alimradi tu ziwe zimerekodiwa Brazil na wahusika ni wachezaji kutoka kwenye timu zinazoshiriki Kombe la Dunia.
6.    Ni marufuku kusifia muonekano wa Cristiano Ronaldo. Kinachomhusu hapa ni soka tu!
7.    Kama umepitwa wakati wa kutambulishwa majina ya wachezaji, tafadhali usiniulize, "yule ni nani?"
8.    Unapaswa kusoma sheria za soka kabla ya kuanza kutizama Kombe la Dunia. Maswali kama, "Mbona au Ni nani yule jamaa anakimbia karibu ya kiwanja akipepea kibendera?" hayatavumiliwa.
9.    Kwa kipindi kizima cha Kombe la Dunia, rimoti itakaa kwenye mfuko wangu na itatumiwa na mimi tu ama kwa ruhusa ya maandishi kutoka kwangu.
Nadhani tumeelewana.

Asante.

Baba Mwenye Nyumba!

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!