12 June 2014

 

Moto mkubwa umetetekeza kabisa soko kubwa la mitumba la karume huko Dar es Salaam usiku wa Jumatano, na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara wote wa soko hilo.

Wazima moto walifanikiwa kuudhibiti moto uloweza kufikia karibu na kiwanda cha kutengeneza bia cha Breweries, lakini haujasababisha hasara yeyote katika nyumba za jirani wa soko hilo kufuatana na mwandishi habari wa Raia Mwema Mbaraka Islam alipozungumza na Sauti ya Amerika.

Anasema hakuna kibada cha biashara kilichosalimika na hakuna mtu aliyefanikiwa kuokowa mali yake. Mfanya biashara Wilson magembe anasema amepoteza kila kitu na ilikuwa vigumu kuweza kuchukua bidhaa zao kwa sababu moto uliwaka kwa haraka sana.

Mpaka tunaandika habari hizi, haijajulikana bado thamani ya vitu vyote vilivyo ungua na kama kuna fidia au msaada wowote toka serikalini, ili kuwakimu na kuwapa angalau kifuta machozi, wachuuzi wa soko ilo.

 


Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!