9 March 2014

 

Mbunge Irungu kang'ata anaongoza juhudi za kundi lililoundwa la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini kenya.sheria zilizopo zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika tabia za ushoga na adhabu yake ni miaka 14 jela.

Huenda ikawa ni nchi inayofuata yenye utata unao husiana na wapenzi wa jinsia moja, huku wabunge wakipanga kuwasilisha muswada bungeni kushinikiza serikali kufanya juhudi zaidi kutekeleza sheria zilizomo za marufuku ushoga.

Kwa upande wao wanaharakati wa kutetea wapenzi wa jinsia moja wanasema shinikizo limeongezeka tangu nchi jirani ya uganda ilipopitisha sheria dhidi ya mashoga mwezi oliopita.

Irungu Kang'ata ambaye ni mbunge kwa mara ya kwanza anaongoza juhudi za kundi lililoundwa majuzi la kupinga wapenzi wa jinsia moja nchini kenya.katika kampeni za wazi kabisaa, mbunge huyo ameomba chama tawala kuelezea serikali inachukua hatua gani kutekeleza sheria zilizopo dhidi ya mashoga.

Sheria zilizopo nchini kenya zinasema ni hatia kwa watu kujiingiza katika sheria za ushoga na adhabu yake ni kifungo cha miaka 14 jela.

Kundi hilo linalo pinga wapenzi wa jinsia moja liliundwa majuzi na raisi wa nchi jirani ya uganda Yoweri Museveni alipotia saini dhidi ya wapenzi wa jinsia moja mwezi February, licha ya shinikizo kutoka katika nchi za Magharibi asitie saini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!