Masjid Musa Mombasa Kenya
Msikiti ilioko Maeneo ya majengo ukijulikana kwa jina la Masjid Musa, kumetokea vurugu kati ya Askari na waumini na kupelekea askari kupiga mabomu ya machozi na wengine kupigwa risasi za moto...
Habari zinasema kuwa askari walipata taarifa kuwa kuna kundi la vijana likiendesha mafunzo ya kijeshi msikitini, kitu ambacho hakikuwa cha kweli.
Habari zinasema kuwa askari walipata taarifa kuwa kuna kundi la vijana likiendesha mafunzo ya kijeshi msikitini, kitu ambacho hakikuwa cha kweli.
Polisi walivamia msikiti na kuanza kumimina risasi za moto kuwaelekea waumini walioko ndani ya msikiti, na fujo zikasambaa maeneo ya majengo kwa muda wa saa nne nzima.
Waislam wapatao mia (100) wamekamatwa, raiya kadhaa wamepigwa risasi za moto. Polisi wawili wameumia mmoja akiwa maututi, inasemekeana walimkuta maliwatoni akiugulia uku akiwa amelala kwenye dimbwi la damu, inasemekena baada ya polisi kuvamia msikitini mmoja wa polisi hao alikamatwa na waumini katika kujitetea na wakamchina bafuni.
Source: Reuters
0 comments:
Post a Comment