27 February 2014

Wanawake Uganda Waandamana Kumpinga Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Baada ya rais Yoweri Museveni wa Uganda kupitisha sheria ya marufuku kwa wanawake Kutembe utupu barabarani, na kutaka wanawake wa nchi hiyo kujistili miili yao.

Polisi wa Uganda wamezuia kundi la wanawake waliopanga kuandamana kupinga sheria inayopiga marufuku picha chafu.

Chini ya sheria hiyo ni marufuku kwa wanawake kuvalia mavazi mafupi, yenye kubana mwilini kiasi cha kuonekana mapaja na makalio na sheti inayoonyesha matiti.

Wanawake hao waliopanga kuandamana mjini Kampala walibeba mabano kupinga sheria mpya uku baadhi wakiwa wamevalia mavazi mafupi. Baadaye walikubaliwa kukusanyika katika uwanja nje ya ukumbi wa kitaifa.

Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
Reactions:

0 comments:

Post a comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!