4 February 2014

Kesi ya kwanza kuhusu mauaji ya kimbari kufanyika nchini Ufaransa imeanza mjini Paris, Ufaransa huku aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi nchini Rwanda akifikishwa kizimbani.

Pascal Simbikangwa anakabiliwa na mashitaka yanayohusiana na maujai ya halaiki nchini Rwanda miaka ishirini iliyopita ambapo maelfu ya watu waliuwawa.

Amekanusha madai hayo.

Waziri wa haki wa Rwanda ameisifia hatua hiyo na kuitaja kesi hiyo kama ya kipekee lakini lakini amesikitika kwamba imechukua muda mrefu kufikishwa mahakamani.
Pascal Simbikangwa anatuhumiwa kwa kosa la kuchochea mauaji ya watu wa kabila la Tutsi, ubakaji , kuwatesa watu na kuwatendea unyama watu hao.

Akitumia kiti cha magurudumu, kapteni huyo wa zamani katika serikali ya aliyekuwa Rais Juvenal Habyarimana, alijulikana kama afisaa aliyeogopewa sana na mwenye kuwatendea watu unyama.

Kabla ya kutoroka Rwanda baada ya mauaji ya kimbari, Bwana Simbikangwa alikuwa mkuu wa shirika la ujasusi alilojiunga nalo baada ya kupatwa na ajali kiasi cha kupoteza miguu yake mwaka 1986.

Bwana Simbikangwa anatuhumiwa kwa kuunda vikundi vya vijana waliofanya mauaji na kuchapisha orodha ya majina ya watutsi waliotakiwa kuuawa mwaka 1994.

Aidha aliomba hifadhi mjini Mayotte, eneo linalotawaliwa na Ufaransa katika bahari hindi ambako alikamatwa mwaka 2008 baada ya kupatikana na stakabadhi bandia za usafiri.
Shirika la polisi wa kimataifa la Interpol, lilipokea taarifa za kukamatwa kwa Simbikangwa na mara moja akashitakiwa kwa tuhuma za uhalifu wakati wa mauaji ya kimbari.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikiituhumu serikali ya Ufaransa kwa kujikokota katika kuwafikisha mahakamani washukiwa wa mauaji ya Kimbare wanaoishi maeneo yake.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!