11 February 2014



Serikali imesaini makubaliano na wadau ya Bandari ya Dar es Salaam, kufanya kazi kwa saa 24 kuongeza ufanisi na utendaji kazi.

Makubaliano hayo yalisainiwa kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaban Mwinjaka na wadau wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Madeni Kipande.

Wadau wengine ni Wakala wa usafirishaji mizigo bandarini (TAFFA), Wakala wa vipimo (WMA), Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Kampuni ya Kuhudumia Kontena Bandarini (TICS) na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA).

Mwanjaka alisema eneo maalumu limeshapatikana kwa ajili ya benki ambapo kwa sasa CRDB na NMB tayari zimepewa eneo lakini pia benki za kimataifa.

Alisema pia nchi nyingine ambazo zinachukulia mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, zinatafutiwa eneo kwa ajili ya kufanyia kazi zingine za msingi wakiwa bandarini hapo.

Kwa upande wake, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga alisema, makubaliano hayo yabane pande zote mbili Serikali na wateja ikiwa mmoja kati yao atabainika kuchelewesha mzigo apigwe faini.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!