28 December 2013


Binti wa miaka 19 ambaye
aliacha shule baada ya baba na
mama kufa katika ajali mbaya na
ndugu kutompa msaada aliamua
kuondoka nyumbani na kwenda
kuishi na kijana mmoja. 

Miaka 10
sasa amekuwa anakaa na rafiki
yake wa kiume avutaye bangi
katika ghetto.
Amekuwa anapewa fedha
kidogo kutoka kwa huyo mpenzi
wake ili anunulie chakula na kula
na marafiki wa kaka huyo baada
ya kutumika kimapenzi kwa wiki
zima huku akiuza maji ya
kunywa.

Baada ya muda akajikuta ni
mjamzito na huyo kijana
akamwambia watoe tu mimba
hiyo.Akampa fedha kidogo na
kumwambia aongeze nyingine
ambazo amekuwa akimpa ili
akatoe mimba bila kukumbuka
kuwa fedha hizo zimekuwa
zikitumika kwa ajili ya chakula.

Siku ya pili yake akiwa anatoka
chumbani mwao kwenda kutoa
mimba, akpita kwenye korido
ambako akakanyanga sakafu
ambayo ina maji na kuteleza. yule
kijana akamwona wakati
anaangukia tumbo pale sakafuni
na akasema, “ amini au usiamini
hii ndio njia rahisi niliyoitaka
uitumie kutoa mimba hiyo”
Kijana akamchukua binti wakati
huo damu nyingi zikimtoka na
kumwambia aende bafuni
akanawe.

Lakini kwa nguvu za
mwenyezi Mungu yule dada
alipona ingawa mimba ilitoka na
akaumwa kwa zaidi ya wiki bila
msaada wowote ule.

Siku moja akiwa anauza maji
akakutana na muuza magazeti
na kumpa maji pakiti moja bure
na kumwambia, “leo ni miaka
kumi tangu baba na mama
yangu wafariki katika ajali
mbaya, hivyo sitajali mchumba
wangu atasemaje au kunifanya
nini kwa kutoa maji haya bure,
ila mimi nitatoa maji bure kama
kumbukumbu ya siku hii yenye
simanzi kwangu”.

Akiwa anataka kuondoka yule
muuza magazeti akamwambia
kuwa kuna nafasi ya kazi
sehemu na kuwa atamsaidia
kuandika barua ya kuomba. Yule
dada ailishukuru na akawa
anampigia mara kwa mara yule
muuza magazeti mpaka siku
akaitwa kwenda kwenye usaili.

Siku ya usaili akiwa njiani
anaelekea huko akakutana na
mama mmoja akiwa na gari aina
ya BMW likiwa nimeishiwa
mafuta. Yule dada akamuuliza
mama, Je unahitaji msaada gani?
yule mama akamwambia
nimeishiwa mafuta na sijui cha
kufanya hapa.

 Dada akachukua
kidumu na kwenda mbio
kumnunulia mafuta yule mama
na akarudi na kumpa.
Yule mama alipotaka kumpa hela,
dada akakataa akasema
nimekuona nikamkumbuka
mama yangu hivyo nimefurahi
kukusaidia, kama hutajali
naomba niwahi sehemu.

Kufika kwenye usaili dada
akashangaa kuona kumbe yule
mama mwenye BMW ndio boss
wa ile kampuni na akafanyiwa
usahili na kuanza kazi na sasa
anajimudu kifedha na ana
biashara zake.

Na sasa hakai tena na yule kijana
mvuta bangi wakati nusu ya
utajiri wake anaupeleka kwenye
vituo vya kulelea watoto yatima.
Nami leo nakuombea
unayeisoma habari hii, Mungu
akujalie na kukufungulia milango
ya mafanikio katika kila jaribu
unalolipitia na ukumbuke
kuwasaidia wanao hitaji msaada
wako.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!