1. Kutokuwa na hofu ya Mungu. Binti huenda kanisani wala msikitini upo tu nyumbani. Mvulana serious akikuangalia ataona ni mtu wa kutumika tu na si mtu unayeweza kulea watoto katika misingi ya maana na kuwa muhimili wa familia.
2. Masaa 24 wewe uko kwenye simu na TV. Ukitoka channel hii unahamia ile. Tamthilia zote unazijua wewe. Hebu niambie kichwa chako kitakuwa kimejaa nini zaidi ya mapenzi ya Kifilipino na Kimeksiko ya kwenye hizo tamthlia?...
3. Hutaki kufanya majukumu ya msingi ya kike kama kupika na kuosha vyombo, kisa TV na sinema zimekuonyesha kuwa hayo pia ni majukumu ya wanaume. Hii ni Afrika mama, utaumia. Unaenda kwa mpenzi wako kumtembelea vyombo unakuta vichafu huoshi, unakaa tu. Unajishushia pointsi. Osha na mwambie si vizuri kuacha vyombo vichafu.!
4. Kuwa mtumwa wa kila kitu kipya. Mtu gani atapenda kuwa na mwanamke ambaye ni mtumwa wa kila aina mpya ya simu, kila aina mpya ya kiatu, kila aina mpya ya nguo, kila saluni mpya anataka kwenda?
5. Kutumia vipodozi hadi unapitiliza. Badala ya kuvutia unatisha!
6. Muda mwingi kutumia kwenye mitandao. Mara Twitter, Mara Facebook, mara Instagram! Wataalam wanasema binadamu ana uwezo wa kuwa na marafiki si chini ya 150 tu. Lakini wewe kila mtandao una watu 2,000! Sasa hivi unaweza kuona haina maana ila ngoja ufike miaka 35 ukiwa single and searching ndo utaelewa.
7. Acha kutoa namba yako kwa kila mwanaume! Hakuna mwanaume ambaye anataka kuwa na mwanamke ambaye kila muda anawasiliana na watu hata wasioeleweka.
8. Jipe thamani na ongeza thamani kwenye maisha ya mpenzi wako. Kama uko shule soma, kama unafanya kazi fanya vizuri, kama una biashara jitume na kila mara mshauri vizuri mpenzi wako. Hakuna mwanaume anataka kukaa na mwanamke ambaye yupo yupo tu!
9. Acha tabia ya kila saa kuruhusu marafiki zako kuongoza maisha yako. Kuwa na misimamo yako.
10. Kutembea tembea na makundi ya wasichana wenzako kila mahali. Kwani lazima? Huwezi kutembea mwenyewe? Inawezekana kabisa katika kundi la wasichana wenzako yuko ambaye ana tabia za ajabu na mwanaume akimuona tu na wewe atakuhukumu kwa kuwa mko kundi moja. Sio muda wote ni muda wa kutembea na kundi la marafiki.
0 comments:
Post a Comment