10 November 2013


Mwanaume mmoja nchini China Bw.Jian Feng amemshtaki mkewe mahakamani kwa kumzalia watoto wenye sura mbaya. 

Picha  inamuonesha mke wa Feng alivyokuwa kabla na baada ya upasuaji.

Magazeti nchini China yametawaliwa na habari hiyo kwa takribani wiki nzima sasa. Gazeti la Guangdong limeripoti kuwa Bw.Feng alimvumilia mkewe alipomzalia watoto wawili wenye sura mbaya, lakini alishindwa kuvumilia alipozaa mtoto wao wa mwisho msichana, ambaye Bw.Feng amemwita ni "Mbaya kupindukia" (an extremely ugly baby girl).

Baada ya kuzaa watoto hao wenye "sura mbaya" wakati wazazi wao wote ni wazuri wa sura, Bw.Feng aliamua kwenda kupima DNA ili kuhakiki kama watoto hao kweli ni wake. Mtandao wa "DAD ALL DAY" unaripoti kuwa vipimo vilionesha watoto wote ni wa Feng. "DNA tests proved that the girl and all of his kids were in fact his."

Baada ya hapo Bw.Feng alifanya uchunguzi na kugundua kuwa watoto wale walichukua sura ya mama yao ambae alikuwa "mbaya kupindukia" kabla hajafanya upasuaji wa kurekebisha sura yake.

Gazeti la Guangdong linaripoti kuwa mwanamke huyo alifanya upasuaji wa kurekebisha sura yake "plastict surgery" nchini Korea Kusini, kwa gharama ya Dola 100,0000 za Kimarekani, sawa na Sh.Milion 160 za kitanzania. 

Lakini hakuwahi kumwambia mumewe Feng kuwa amefanyiwa upasuaji wa kurekebisha sura. "she had undergone over $100,000 in plastic surgery in South Korea before met Feng and never told him" Linaripoti gazeti la Guangdong.

Mahakama mjini Beijing ilivunja ndoa hiyo baada ya Feng kudai kuwa hawezi kuendelea kuishi na mkewe huyo, na mahakama imempiga mwanamke huyo faini ya Dola 120,000 sawa na Sh.Mil.190 za Kitanzania, ambazo atamlipa mumewe Feng kwa kumdanganya na kumzalia watoto "wenye sura mbovu"

Picha inayoonyesha familia ya Feng, akiwa na mkewe na watoto aliowalalamikia ni "wabaya" (huyo mtoto mdogo aliyebebwa na Feng ndiye aliyeibua kasheshe). 

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!