6 August 2013


Watoto Noah na Cannor Barthe wakiwa na mama yaoMandy Trecartin
Watoto wawili wa kiume wanaotambulika kwa majina ya Noah Barthe mwenye umri wa miaka mitano(5) na kaka ake Cannor Barthe mwenye umri wa miaka saba(7)wameuawa baada ya kushambuliwa na nyoka aina ya python.

Watoto hao walishambuliwa na nyoka huyo wakati walipokuwa wamelala katika flat ya rafiki yao katika mji wa Campbellton nchini Canada.

Watoto hao walikuwa wamelala sebuleni,wakati wanapata shambulio la nyoka huyo jana asubuhi.

Mnyama huyo ambaye alikimbia katika sehemu ya kuuzia wanyama inayoitwa Reptile Ocean pet store ambayo inamilikiwa na rafiki wa familia Yao bwana Jean Claude Savaie,ambayo ipo ghorofa ya chini ya jengo ambalo watoto Yao walikwenda kulala.

Bwana Savoie amelimbia Global News kwamba aliona kitu cha kutisha asubuhi saa kumi na mbili asubuhi wakati anakwenda kuwaangalia watoto hao.

''Nilifikiri wamelala lakini nikaona tundu juu ya paa,na kila kitu kilikuwa kimeshatokea,nikawasha taa na nilichokiona ni kitu cha kutisha sana na siamini Kama ni kweli''alisema bwana Savoie

Mama wa watoto hao Mandy Trecartin, ambae anaishi karibu na duka hilo la kuuzia wanyama la  Reptile Ocean store.

Polisi wamesema nyoka huyo anaetambulika kama Afican rock python aliingia katika juu ya ghorofa hilo kupitia store mbili za ghorofa hilo.

 Uchunguzi wa awali wa polisi unasema python alifanya shambulio hilo baada ya kutoroka katika duka Hilo la kuuzia wanyama.

''Inaonaoneka nyoka huyu aina ya African python alipanda juu ya ghorofa kupitia store,na ninaamini watoto hawa walipata tabu sana kwa kushambuliwa na nyoka huyu.alisema Msemaji wa polisi 

Nyoka huyo aina ya Afican rock python amepatikana kwa uchunguzi zaidi.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!