27 May 2013


Mahitaji
Kuku mgumu mmoja
Nyanya kopo moja
Vitungu maji vikubwa viwili
Vitunguu swaumu punje nne
Tangawizi mbichi kiasi
Tomato pure kijiko kikubwa cha chakula
Pilipili boga tatu rangi tofauti tofauti
Viazi mbatata(baby potatoes)
Chumvi kijiko cha chai kimmoja
Limau moja/ndimu

Jinsi ya kupika
Katakata kuku wako muoshe mbandike jikoni muweke limau chumvi,tangawizi na kitunguu swaumu,mfunike achemke na yale yale maji uliyomuoshea.
Yakikaribia kukauka weka vitunguu maji ukivyovikatakata na yale mapilipili boga,weka nyanya na tomato pure,osha viazi vyako vitumbukize wacha kwa dk tano.
Taarisha tray yako ya oven,iweke foil mimina mchanchanganyiko wako wa viazi na kuku ktk tray,weka ktk oven kwa nusu saa moto 180

Bado hakijaingia ktk oven
Kimeshaiva


Tayari kwa kuliwa
Unaweza kuandaa kwa mchana au jioni
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!