3 April 2013


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salma Kikwete,ambae pia ni Mwanaharakati wa Kijamii kupitia Chama Chake cha Wanawake na Maendeleleo, wiki iliyopita alizawadiwa Nishani na Chama kinachojishughulisha na kuinua kiwango cha Elimu kwa Nchi za Afrika Mashariki kilichoko katika jiji la London, Uingereza.

Mke huyo wa Rais wa Tanzania alitunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake mkubwa wa kuinua Elimu ya Mtoto, hususan wa kike na kumuwezesha mwanamke ili aweze kujitegemea kimaisha.

Akizungumza katika Hafla hiyo iliyofanyikia katika kumbi za Hoteli ya Park Plaza iliyopo pembeni mwa Westminster Bridge (katikati ya jiji la London) Dr Mohammed Zaharan ambae ni Katibu wa Chama hicho cha East Africa Education Foundation (EAEF) alisema kuwa Chama Chake kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu na  shughuli zinazofanywa na Mama Kikwete kupitia Jumuiya ya WAMA.

Dr Zaharani aliongeza kuwa Mama Kikwete ni mfano bora na  wa kuigwa na Wanawake katika jamii ndani na nje ya Tanzania.

Naibu Spika Mh. Job Ndugai na Mbunge Mama Beatrice Shelukindo wakipokea nishani hiyo kutoka kwa Dr Mohammed Zaharani (katikati yao )  kwa niaba ya Mama Salma Kikwete .  Pembeni wa kwanza ni Nd. Haruna Mbeyu maarufu kama Meya wa London na anaefuatia kabla ya Mh. Mama Shelukindo ni Bi. Mariam Mungula , Katibu wa Tanzania Women Association (TAWA) UK.


Akipokea Nishani hiyo kwa Niaba ya Mama Salma Kikwete, Naibu Spika Mh. Job Ndugai  (Ambae alikuwa Nchini Uingereza kwa Mualiko wa Naibu Spika wa Uingereza na aliongoza na Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utumishi ya Bunge) alisema kuwa amefurahishwa sana na kitendo hicho cha Mchango wa Mama Salma kuonekana, kwa kuwa kinadhihirisha mchango unaofanywa na Jumuiya zisizo za Kiserikali katika jamii kama WAMA unaonekana mpaka Nje ya Tanzania.
Mh. Naibu Spika Job Ndugai akipokea Nishani hiyo kutoka kwa Dr. Mohammed Zaharani . Wakiangalia kwa furaha ni Mh. Beatrice Shelukindo, Bi Mariam Mungula na Nd. Haruna Mbeyu

Baadhi ya Akina Mama waKitanzania waliohudhuria hafla hiyo katika picha ya upendeleo na M. Beatrice Shelukindo na Nishati ya Mama Salma .
Awali Mh.Beatrice Shelukindo alisema ni jambo kubwa na kufurahia sana 
na linadhihirisha mchango mkubwa wa Mama Salma katika kumuendeleza Mwanamke wa KiTanzania na inatia moyo kwa Wanawake Wengine.

picha na habari:Jestina George

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!