15 April 2013

Wema na Mama yake

My gal huu ni Ushauri wa bure ninakupa.
Wema hivi ulishindwa kutafuta watu ndani ya familia yenu mkakaa kulzungumzia kitendo ulichofanyiwa na mama yako hadi ukaamua kumpeleka polisi?siamini kama katika familia yenu hakuna watu wazima,hapa ninamaanisha bibi,babu na wajomba zako?
Wema hakuna rafiki mzuri na wa kweli kama mama yako hapa duniani,hivi utakuwa wa aina gani kama unathamini wa nje huku unamdharau mama yako mzazi,sikulazimishi kufuta kesi ila kaa fikiria mara mia moja halafu toa maamuzi.
Ninafahamu sheria zipo lakini hili la kwako lilikaa kifamilia sana au ndio ulikuwa unakata magazeti yakuandike?hapana wema hakuna umaarufu unakuja kwa kutemtendea mama yako aliyekuzaa mambo ya ajabu.

wema hata wewe ulikaa hivi tumboni kwa bi mkubwa wako

Wema kuna watu wanatamani leo mama zao wangekuwepo walau wakawaadhibu kama wewe ulivyoadhibiwa na mama yako lakini hawapo,wema wacha nikukumbushe hakuna mtu wa kuthamaminiwa hapa duniani kama mama yako,mama yako ndio maisha yako,mama yako ndio pepo yako kwa mwenyezimungu.
Wema ikiwa tunaambiwa tukibusu miguu ya mama zetu tu tunaingia peponi vipi wewe amabe unashindwa hata kumnyenyekea mama yako?
Hivi kweli ulishindwa kukaa na mama yako mkazungumza wewe umeona njia nzuri ni kumpeleka polisi?
Unasahau kama huyo ndio mwanamke aliyekuweka tumboni miezi tisa?
Hata kama atakuwa na makosa mama ni mama kuna njia za kuongea naye ila si kumpeleka polisi.
Inawezekana Mama Wema anamapungufu yake ila kitendo cha kumpeleka polisi mama yako si cha heshima umemchukulia kama alivyo mtu mwingine yoyote hujamchukulia kama mama yako au kuna siri chini ya pazia? Pengine mnachukuliana mabwana?
Unataka kuniambia hivyo vitu alivyovunja vina thamani kuliko mama yako mzazi?Kwetu sisi wewe ni star ila kwa mama yako wewe ni mtoto tu.
 Wema tambua kuwa wewe kwa mama yako sio star,na pia maisha yako hayatakuwa na maana kwa kuandikwa kwenye magazeti tena bila ya kulipwa  shilingi nyekundu,kwa hil;i wema umejitia aibu kubwa.
Tambua kila unalomfanyia mama yako nawe utakuja kufanyiwa na watoto wako.
Nimemaliza.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!