28 March 2013






Mbunge wa Chambani-Pemba, Kisiwani Zanzibar Salim Hemed Khamis ambaye jana aliugua ghafla wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ofisi ndogo jijini Dar es Salaam Amefariki.

Khamis,mara baada ya kugua ghafla alisaidiwa na Wabunge wenzake na Maofisa wa Bunge na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kwa matibabu na mchana huu amefariki dunia.



Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.Salim Hemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo jana jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.

Taratibu za kuusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.

habari na picha kwa hisani ya Father Kidevu Blog

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!