27 January 2012

Miaka ya hivi karibu mitindo ya nguo na muonekano wa mwanaume umebadilika sasa wabunifu wanawabunia vitu kama wanawake hapa niongelea katika suala zima la uvaaji na utengezaji wa nywele yaani muonekano kiujumla.
Katika sehemu za matukio au mikusanyiko  zamani wanaume au wavulana walikuwa na furaha kwa kuwa walikuwa na nguo za kueleweka,lakini sasa kila kitu chao kimebadilika wanaonekana kama wanawake katika uvaaji kutokana baadhi ya wabunifu wa nguo za kiume sasa kubuni nguo hizo zikiwa zimefanana na za kike.Mitindo ya uvaa wa wavulana/wanaume sasa zimekuwa sio fulana na suruali,kwani nguo zao sasa zimekuwa zikifanana na za kike zaidi ya zamani,hapa ninajumlisha na jinsi ya utengezaji wao wa nywele pia ulivyobadilika,kwani nao sasa hupaka hata nywele zao rangi.
kwanza mwanaume/mvulana anatakiwa kuchagua aina ya mtindo wake wa nywele kutokana na muonekano wake alionao.na kitu muhimu cha mwanaume cha kuzingatia katika sula zima la mitindo ni nywele,mtindo wa nywele zako ni lazima uendane na uso wako na muonekano wako umbo,kama hauna uhakika na mtindo gani wa nywele unakufaa ni vyema ukapata ushauri kutoka kwa muhusika wa salon unayokwenda,kwani hapo utapata ushauri mzuri utakao kufanya muonekano wako uwe wa kupendeza na sio kung'ang'ania mtindo ambao haundani na wewe sababu tu mtu fulani umempendeza basi na wewe utakupendeza hapana.Hakikisha nguo unayovaa inaendana na sehemu unayokwenda,kwani wanaume wengi huvaa kibiashara hata sehemu zisizohusika,katika sehemu zinahusu mambo yakibiashara vaa suits ya kueleweka ili ufanananie na sehemu husika.
Utakuta mwanaume mwengine amekwenda katika party ya harusi{ reception}ametinga sare ya timu ya mpira,au amevaa nguo kama na kwenda disco kwa kweli inasikitisha sana.
Pia hakikisha nguo zako ziwe na rangi tofauti sio mashati ya blue unayo sita  na yote yanakaribia kufanana,kiasi hauonekani tofauti unapokuwa umevaa na kupelekea kuonekana kila siku umevaa shati moja.

For casual dating,hapa ni lazima uvae nguo zinazoenda na hili tukio,yaani nguo na viatu ni lazima viwe casual.

Viatu ni kitu muhimu kwa kumfanya mwanaume /mvulana kuonekana maridadi na mwenye kwenda na wakati,hivyo hakikisha wakati unanunua viatu viwe vile vitakavyokupelekea kuwa huru wakati umevivaa.
Hakikisha kama uwezo unao basi uendane na mitindo mipya kwani  kila siku na kila mwaka mitindo ya wasichana na wavulana  inabadilika.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!