7 January 2015

Kutafuta mtotoni jambo la raha na furaha baina ya mke na mume, kujifungua ni uchungu ambao huwachiwa mwanamke pekee. kulingana na vitabu vitukufu, uchungu unaohisiwa wakati mwanamke anapojifungua ni laana na adhabu kwa wanawake kutoka kwa mungu baada ya Hawa kumdanganya Adam kufanya dhambi.

Mbali na kukaa katika chumba cha kujifungua wanaume wengi hupendelea kwenda mbali ama hata kusafiri wanaposikia wake zao wanataka kujifungua.

Simulizi nyngi zimesikika kuhusiana na wanaume kutafuta sababu za kwenda mbali ama hata kujitafutia visafari wakati wake zao wanapokaribia kujifungua.

Baadhi ya sababu zinazotolewa na wanaume wakati huo ni kwamba hawawezi kukaa ndani ya chumba cha kujifungulia kwa kuwa kitendo hicho ni cha uchungu mwingi na kinatisha.

Je, inafaa kwa wanaume kuingia ndani ya chumba cha kujifungulia na kushudia kitendo cha Mke kuzaa na ikiwezekana kuwasaidia wakunga?

Waweza Kujadili swala ili, kwa kutoa maoni yako au ushauri wako.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!