20 February 2014


Harnaam Kaur, ni binti anayeishi nchini Uingereza. Alianza kuota ndevu akiwa na umri wa miaka 11.

Ili aonekane kama wanafunzi wenzake, alianza kuzipunguza mara mbili kwa wiki ndevu zake zilizokuwa zikimea. Alijaribu hata kuzipausha na kuzinyoa pia.

"Nilikuwa nikichekwa sana,” anasema, kwa mujibu wa gazeti la Mirror la nchini Uingereza. “Shuleni nilikuwa nikiitwa ‘beberu’ na majina kama vile ‘jike-dume’ na kadhalika.’”

Baada ya kubainika kuwa na ovari lenye uvimbe, hali ambayo husababisha ukuaji mkubwa wa nywele kwa wanawake, Kaur anasema alifikiria kujiua wakati wakiwa kijanda mdogo.

Lakini sasa, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23 aliikubali hali yake na anasema: “Nimebadilika sasa na nimejifunza kuikubali hali yangu.”

"Najihisi nimezidi kuwa mwanamke, mrembo na mwenye mvuto,” anasema Kauri. “Nimejifunza kujipenda kwa vile nilivyo hakuna anayeweza kunitikisa kwa sasa.”

Ili kukabiliana na hali yake, Kaur ambaye anafanya kazi kama mwalimu, aliamua kuingia katika dini ya Singasinga akiwa na umri wa miaka 16. Katika dini ya Singasinga wanaamini kuwa nywele za mwili zinatakiwa kuachwa zikue.

Licha ya kutazamwa tofauti na watu wa nje, Kaur anasema kuwa siku zote familia yake imekuwa ikimuunga mkono.

"Kwa kweli kaka yangu ndiye aliyeshtushwa na nilichokifanya,” anasema wakati akisimulia tukio la kuamua kuzikata ndevu zake, “alinikumbatia na kusema kuwa nilionekana mrembo nikiwa na ndevu zangu, hakuelewa kwa nini nilikuwa nimefanya hivyo. Hapo ndipo nilipoamua kuwa sitaziondosha tena.”

"Ninapokuwa dukani wahudumu huniita ‘bwana’ na watu hunitazama kwa mshangao,” anasema.

"Wanaonifrahisha zaidi ni wanafunzi wangu. Baadhi huniuliza ndevu zangu zina nini, nami huwatania kwa kuwaambia kuwa ni mtindo wa Sikukuu.

"Bado sijapata mtu makini wa kunioa. Bado nina huzuni kiasi… nab ado hali hii inaonekana kuwa ni kikwazo cha mimi kuolewa, lakini mimi bado kijana na bado kuna muda wa kutosha kufanya hivyo. Kitu muhimu kwa sasa ni kwamba ninajipenda. Ninazipenda ndevu zangu na kila kitu nilichonacho.”

Source: mirror

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!