Miaka hii ya karibuni tunashuhudia vijana wengi wakiyafurahia mafanikio ya kimaisha. Ukiangalia kwa jicho la kawaida tu, unaweza sema mafanikio yake yametokana na jitihada zake aidha uoneshaji wa mavazi (Modelling) muziki au uigizaji wa video, wenyewe wanaita Bongo Movie.
Hatukatai kuwa hizo zote ni kazi na zinalipa, lakini tusidanganyane kuwa kulipa uko kunaweza kumpelekea mtu akaweza kumiliki gari lenye thamani ya milioni 80, si kweli hapa tunapigwa changa la macho.
Lakini Mungu si Athuman wala si John, wale wote ambao wanaishi as disguise kumbe nyuma ya pazia ni watu hatari sana, tena naweza kusema ni watu wenye roho mbaya kiasi cha kuamua kuangamiza jamii inayomzunguka kwa uhuzaji wa madawa ya kulevya, siku hizi wanaita sembe.
Binafsi siwaonei huruma watu wa namna hii, hata awe maarufu au mzuri wa sura kwa namna ya kipekee, as long yeye ameamua kuingia kwenye biashara ya kuuza madawa ya kulevya huyo ni adui yangu nambari moja.
Utakuta mtu anadiriki kusema “Jamani Kaeni Chini Mfanye Yenu... Mbona Yeye Fulani Alitulia Akafanya Yake!”
Mtu kama huyu tumuweke katika kundi gani? Kama hausiki na haya madude kwa namna moja au nyingine basi anafaidika nayo na hizi ni dalili za ubinafsi uliopindukia mipaka, mtu mmoja anajitahidi kutoka kimaisha kwa kuwaangamiza wengine, kisha anaangukia pua, pembeni anasifiwa kuwa kajitoa muhanga, tukiwa na fikra hizi nchi hii itaendelea kuangamia kila upande, viongozi mafisadi, baadhi ya raiya wachache wanakimbilia kuuza sembe ili kuangamiza walalahoi wenzao... Kisha tunasifia dah! Jamaa katokelezea kichini mtu wangu...!
Hatuwezi kukaa pembeni na kusema kuwa “Kila mtu na maisha yake” uku wanao athirika ni ndugu, jamaa na marafiki na majirani, ubinafsi huu ndio umepelekea vijana wengi kuwa vibaka, wezi au majambazi… Sababu ndio hii ya kila mtu ajali mambo yake… Kuna mambo binafsi ambayo uwezi kuyaingilia, lakini swala linapokuwa linahusu jamii yetu hatuna budi kuyakemea kama si kuyazuiya kabisa.
Je ni sawa kutojali maisha ya wenzentu, kiasi cha kuona mtoto wa jirani akiharibikiwa na kutizama tu, bila kuchuwa hatua zinazofaa? Japo kunyayua kinywa na kutamka kwa kuonya kuwa anachofanya si kizuri? Nasema tena… Wenye tabia hiyo MKOME...!
Binafsi sioni sababu ya kuona huruma kwa mtu ambaye amekamatwa kwa kubeba madaya ya kulevya, kwa sababu angefanikiwa angepelekea kuharibu nguvukazi ya vijana.

Umefika wakati sasa tuseme na njaa zetu...!
0 comments:
Post a Comment