3 June 2012



 Fiona mbwa wa Wema Sepetu Apimiwa Magauni kwa Fundi Cherehani
Wema alitoa maelekezo kwamba anataka Fiona ashonewe nguo za rangi mbalimbali ambazo yeye anazo ili wakitoka wote wawe wanamechisha.

 Wema kwa kweli kitendo hiki kwa imani tu ya dini ni kufuru uliyoifanya,sikuingilii katika maamuzi yako lakini nikiwa na kashibiki wako,na ndugu yako katika imani ya dini,kwa kweli kitenbdo hiki sio kizuri kabisa.

Wema kitendo ulichafanya ni kufuru kwa mwenyezimungu,hebu kaa na ujiulize kuna watoto wangapi vijini ambao hawana hata nguo za kuvaa wewe ukamshonee mbwa  ambaye ameumbwa Mwenyezimungu kuishi mazingira ya kutovaa nguo,tena unajifaragua eti oooh tukitoka tuwe tumevaa sare sare hakika huo ni ulimbukeni wa akili.

Halafu kama mnataka kuiga hao watu maarufu wa huko mbeleni sidhani kama wao wanakwenda na mambwa katika sherehe kama alivyofanya huyo mjengezi mwenzio Irene alipombeba mbwa katika sherehe ya watu,nina waapia laiti sherehe ingekuwa ya kwangu yule mbwa asingeingia kabisa.

Wema wewe ni msichana muelewa na uliyepitia maisha mazuri,usiwe limbukeni na mtu mkosa maadili kwa kumuita mbwa eti ndio mtoto wako.Igizeni vitu vizuri na sio kuiga mambo ya ajabu,au ndio kutaka kuonekana mnaandikwa kila siku katika magazeti ya rangi rangi bila ya kupewa kitu chochote.

Basi hao watu maarufu wenzenu wakiandikwa wanalipwa na sio kuandikwa tu kama mnavyofanya nyie,baada ya nyie mlipwe,nyie ndio mnatoa pesa huu ni ukosefu wa ufahamu kabisa.

picha:global publisher
Categories:

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!