10 February 2012

 Marehemu Christavina na mume wakiwa wanakata keki siku ya harusi yao
---
Familia ya Kusaga inawaomba watanzania wote walioko Marekani na hasa eneo la Washington DC na vitongoji vyake kushirikiana nao katika harambee (fundraising) itakayowasaidia  kuweza kupata pesa ya mazishi ya ndugu yao mpendwa Christavina Kusaga Cryor aliyefariki February 7, 2012 kwa sarakani ya utumbo (Colon Cancer).
Marehemu aliyekuwa akiishi Landover, MD. Ameacha mume na watoto  wawili- mvulana mwenye umri wa miaka 4 na msichana mwenye umri wa miaka 2.

Tafadhali fika tushirikiane ili tuweze kumzika mpendwa wetu Christavina.
  Gharama za mazishi ni $11,000, jumla ya kiasi kilichopatikana hadi sasa $2,000. 
Harambee itakuwa Jumapili February 12, 2012, kuanzia saa 8.30 mchana (2.30pm).
Anuani ni: 3621 Campus Drive, College Park, MD 20740.
Kwa walio mbali au kwa watakaoshindwa kuhudhuria tunaomba tafadhali wasilisha mchango wako kwa kutumia Capital One Bank, Account# 1351500235; Routing # 255071981. Tafadhali kila mwenye kuona tangazo hili amjulishe na mwenzie.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na watu wafuatao: Magoma (202.607.1976); Adelaida (240.602.3183); Matinyi (301.792.2832); Mkakile (240.938.3177); Teddy (301.25441696); Makaya (202.460.1044); Latifah (240.603.7353); au Rebecca (202.580.4648). 
Tunatoa Shukran za dhati kwa wale wote waliokwisha kutoa michango yao na wale wanaoendelea kutoa.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.AMINA

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!