25 January 2012

Usiku wa jana majira ya saa 8 usiku  nikiwa natoka kwenye mizunguko yangu nikielekea home Mbezi kwa Msuguri, nilipofika maeneo ya Kimara resort nikakuta mtu ameanguka barabarani huku pikipiki ikiwa juu yake, nikasimama ghafla kwa umbali wa kama mita 10 nikiwa na tathimini kama ni kweli ninayoiona ni ajali. 
Nilipokuwa napepesa macho kwa pembeni ya barabara nikamuona mtu mwingine kalala chali nikajiridhisha kwamba watakuwa wameanguka na yule kutupwa. 
Nikashuka kwa tahadhari niliposogea km hatua tano nikakumbuka nyuma kidogo nilipita pikipiki ilipokuwa imeegeshwa pembeni bila ya mtu juu  nikashtuka na nilipogeuka kwa mbali kizani nikaiona inakuja kimya kimya bila kuwashwa  na bila mwanga nikagundua utakuwa mtego.


Kwa speed ya rocket nika rudi kukimbilia gari yangu na ndipo mwenye pikipiki naye akawasha kuja kuniwahi, ikanibidi ni mtishie kama nina mrukia akanikwepa na mimi nikarukia kwenye gari yangu. 
Kwa kuwa ilikuwa silence nika tia gear nikiwa tayari kuwagonga kama wangejaribu kunibugudhi mara wale wengine nao wakadandia yao nakuanza kukimbia nikajaribu kuwafukuza niwagonge japo kidogo wakaingia barabara ya vichochoroni nikajirudia zangu.


Jamani hii ndo Tz yetu sasa, msaidie tu yule unayemfahamu.
By Macmillan George
source father kidevu

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!