12 March 2015



Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Happy au mama Hassan, mkazi wa Mbande jijini Dar, wiki iliyopita yalimpata mazito kufuatia kutumbukia kwenye shimo la choo lililokuwa katikati ya chumba anachoishi kwenye nyumba aliyopanga.

Tukio hilo lilitokea wakati mwanamama huyo akifanya usafi chumbani humo na kujikuta akitumbukia kwenye shimo hilo ambalo awali lilikuwa la choo.

MSIKIE MWENYEWE

“Nimeishi hapa kwa zaidi ya mwaka sasa lakini sikuwahi kujua kama katikati ya chumba changu kulikuwa na shimo la choo. Mbaya zaidi nimetoka kumlipa baba mwenye nyumba pesa yake ya kodi juzi tu kwa kipindi kingine.”

“Siku ya tukio niliamka vizuri nikaanza kufanya usafi kama kawaida, ghafla nikajikuta natumbukia kwenye shimo. Ilibidi nipige kelele za kuomba msaada maana ilikuwa mshtuko kwangu,” alisema mwanamama  huyo.

Anaendelea: “Wapangaji wenzangu waliposikia kelele walikuja kunisaidia, walitumia ngazi mbili nikaweza kutoka wakanikimbiza katika zahanati ya karibu kwa ajili ya matibabu maana nilichubuka sehemu mbalimbali za mwili.”

ALICHOSEMA BABA MWENYE NYUMBA

“Mpaka natolewa kwenye shimo baba mwenye nyumba hakuwepo, alitafutwa akaja na kunitaka nisiende polisi tuyamalizie nyumbani lakini hakunipa hata shilingi ya kusema itanisaidia matibabu,” alisema mama Hassan.

“Baada ya ajali hiyo, kuna mtu aliniambia kuwa, awali chumba changu kilikuwa choo. Baba mwenye nyumba aliamua kuziba kwa kuweka sementi kidogo juu ili kuziba tundu lakini pia bado sehemu kubwa ya choo ilikuwa dhaifu ndiyo maana nilitumbukia.

“Aliamua kuziba choo ili kiwe chumba cha kupanga, akachimba choo sehemu nyingine.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!