19 February 2014


Kichinjio cha kwanza cha Punda nchini Kenya kinatarajiwa kuanza kutumika mwezi Machi wakati kitakapokamilika.

Wakaazi wa mji wa Naivasha nje kidogo ya mji mkuu Nairobi watakuwa wa kwanza barani Afrika kuwa na kinjichio cha punda ambao wamekuwa wakiwatumia kwa kukeba maji.

Aidha wakaazi hao hata hivyo wamekuwa wakipata hasara kubwa kwani Punda wao ambao huwatumia kubeba maji wamekuwa wakiibwa na kuchinjwa kisiri huku nyama yake ikiuziwa wateja wasiokuwa na habari kuwa wananunua nyama ya Punda.

Kwa muda mrefu mizoga ya wanyama hao imekuwa ikipatikana kando ya barabara au msituni ambako wezi huificha baada ya kuwachinja Punda hao.

Lakini sasa haya yote yatakuja kuisha baada ya mradi wa ujenzi wa kichinjio cha Punda kuanza mjini humo.

Kichinjio hicho kitakuwa cha kwanza na cha kipekee Kenya na Afrika Nzima cha nyama ya Punda.
Taarifa zinasema kuwa nyama hiyo tayari ina hitaji kubwa nchini China.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!